Mwigizaji aliyekwenda hewani Bongo, Miriam Jolwa
‘Jini Kabula’ amemtaka mzazi mwenziye, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ aoe
ili kulinda heshima yake.
Mzazi mwenza wa ‘Jini Kabula’, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ akipozi.
Akizungumzia maisha yake ya uhusiano mbele ya mwanahabari wetu,
Kabula alisema anajivunia kuzaa na Chuz lakini kwa kuwa yeye hakupanga
kuolewa na prodyuza huyo mkongwe, ni bora aoe kwani umri unamtupa mkono.
“Chuz aoe tu sasa umri umeenda. Tena akioa mimi nitacheza muziki
balaa siku hiyo, si unajua mambo yangu. Mbaya zaidi sina kabisa wivu
naye,” alisema Jini Kabula.
إرسال تعليق