Jeshi la wananchi nchini (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi
na usalama nchini limeahidi kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa
kuwa majambazi sugu ambao wanapora silaha za askari huku wengine
wakiuawa hatua ambayo imeanza kutishia usalama wa nchi.
Akizungumza na jijini tanga kufuatia hivi karibuni makundi hayo
kupora silaha na kisha kuua askari huko rufiji mkoani pwani na wengine
wakipora askari wawili silaha nyakati za usiku jijini tanga na kisha
kuwadhuru hatua ambayo imesababisha kulazwa katika hospitali ya rufaa ya
mkoa wa tanga bombo,katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga
taifa JOB MASIMA amesema vyombo vya ulinzi vitakaa na kuhakikisha kuwa
mtandao huu unapatikana ili kurejesha silaha hizo.
Hata hivyo katibu mkuu amekana vikali kuwa huenda makundi haya ya
uhalifu yanayojihusisha na kupora silaha askari kwa na wahitimu
waliopitia mafunzo ya jeshi la kujenga taifa JKT ambao baadhi yao
hawakupata ajira baada ya kurudu uraiani na kuongeza kuwa hata
wanaojihusisha na ugaidi sio wote ambao wamepitia mafunzo ya kijeshi.
إرسال تعليق