Mafuriko Malawi, 200 wafariki

Serikali nchini Malawi imesema kuwa inaendelea kufanya jitihada za kuwaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko makubwa yaliyotokea katika nchi hiyo.
Baada ya vikosi vya uokoaji kuzidiwa ilililazimu jeshi la nchini humo kuingilia kati siala la uokoaji na kuanza  kutumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.
Hadi hivi sasa Serikali ya Malawi imethibitisha kuwa Takriban watu 200 wameripotiwa kufa na wengine  200,000 wakilazimika kuhama makwao.
Kufuatia hatua hiyo Serikali ya Msumbiji pia imeingilia kati juhudi za wokozi, hata hivyo  Serikali hiyo imeomba msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathira chakula maji na makao.

Post a Comment

Previous Post Next Post