Serikali nchini Malawi imesema kuwa inaendelea kufanya jitihada
za kuwaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko
makubwa yaliyotokea katika nchi hiyo.
Baada ya vikosi vya uokoaji kuzidiwa ilililazimu
jeshi la nchini humo kuingilia kati siala la uokoaji na kuanza kutumia
mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka
kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.
Hadi hivi sasa Serikali ya Malawi imethibitisha
kuwa Takriban watu 200 wameripotiwa kufa na wengine 200,000
wakilazimika kuhama makwao.
Kufuatia hatua hiyo Serikali ya Msumbiji pia
imeingilia kati juhudi za wokozi, hata hivyo Serikali hiyo imeomba
msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathira
chakula maji na makao.
إرسال تعليق