Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi
waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile
kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph
Kabila.
Watu kadha walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na
majeraha ya risasi ambapo pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha
mji huo.
Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma.
Watu
kadhaa walipatikana na majeruhi ya risasi katikati mwa mji huo huku
ghasia zengine zikiripotiwa katika katika chuo kimoja kikuu.
Viongozi wa upinzani waliitisha
maandamano hayo baada ya bunge dogo kuidhinisha sheria siku ya jumamosi
inayoagiza kufanyika kwa hesabu ya idadi ya watu kabla ya uchaguzi wa
urais utakaofanyika mwaka ujao.
Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa mpango huo utachelewesha uchaguzi huo ambao umekuwa ukingojwa kwa hamu kwa miaka kadhaa.
Rais
Joseph Kabila ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15 amehudumu miula
miwili na hawezi kuwania tena urais kulingana na katiba.
Bunge kuu linatarajiwa kuungazia mswada huo wa uchaguzi hii leo
إرسال تعليق