Makumi ya watu wamepoteza maisha yao kufuatia mapigano yaliyotokea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kanali Felix Basse Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa
Mataifa nchini Kongo (MONUSCO) amesema kuwa, watu wapatao 30 wameuawa
na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano ya juma lililopita
kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa Patriotic Resistance Force of
Ituri.
Taarifa ya MONUSCO imebainisha kwamba, 24 kati ya waliouawa katika
mapigano hayo ni wanachama wa kundi hilo na waliobakia ni askari wa
Congo Kinshasa.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, eneo la mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini, daima
limekuwa uwanja wa harakati za makundi ya wanamgambo wa Kikongo na waasi
kutoka Rwanda na Uganda.
Wananchi wa Congo wanayanasibisha machafuko ya mashariki mwa nchi hiyo
na tamaa pamoja na uchu wa mashirika ya kigeni wa kutaka kupora utajiri
wa maeneo hayo.
Post a Comment