MFANYABIASHARA mwanamama aliyetambulika kwa jina la Prisca Paul Rugeiyamu au Mama Koku (34) ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi nje ya geti la nyumba yake huku mwanaye Careen (12) akishuhudia.
Padri akiuombea mwili wa marehemu Prisca Paul Rugeiyamu kanisani.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Januari
12, mwaka huu saa mbili usiku maeneo ya Tabata Segerea jijini Dar
ambapo kwa mujibu wa chanzo, Prisca alikuwa akirejea nyumbani kwake
ndani ya gari aina ya Vitz baada ya kukusanya mapato yake ya siku kutoka
kwenye biashara zake.
Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini.
Akiwa nje ya geti la nyumba yake akisubiri
kufunguliwa, ndipo majambazi walitokea ghafla wakiwa kwenye pikipiki na
kulizunguka gari hilo na kutoa bastola wakitaka wapatiwe fedha na laini
za mitandao ya simu alizokuwa akizitumia katika biashara yake ya huduma
za kifedha kwa njia ya simu katika moja ya maduka yake.
Waombolezaji wakiwa ni wenye huzuni kaburini.
Chanzo hicho kilisema kuwa, Prisca
alibishana na majambazi hao kwa muda ambapo walimpiga risasi ya mguuni
na kumuongeza nyingine baada ya kuendelea kugoma kutoa fedha.
“ Walimpiga risasi nyingine sehemu za tumbo na kuchukua fedha zinazodaiwa kufikia shilingi milioni arobaini na tano huku mwanaye Careen akishuhudia tukio hilo baada ya kufungua geti hilo kwa ajili ya kumpokea mama yake,” kilisema chanzo.

Waombolezaji wakiweka taji la maua kwenye kaburi la marehemu.
Inaelezwa kuwa Careen baada ya kuona hayo alikimbilia kwa bibi yake
ambaye ni mama mzazi wa Prisca anayeishi jirani na nyumba yao aliyefika
eneo la tukio ambapo majambazi hao waliokuwa wakijiandaa kutoweka
walimpiga risasi ya mguu mama huyo na kuondoka kwa kasi.
Hata hivyo, baada ya majirani kufika eneo
hilo walimchukua Prisca na kumkimbiza Hospitali ya Amana lakini
alifariki akiwa njiani na maiti yake ikahifadhiwa hospitalini hapo.
Mtoto wa marehemu akishika picha ya mama yake.
Akizungumza na waandishi wetu, ndugu wa
familia hiyo anayejulikana kwa jina la Geofrey Frank alisema kuwa baada
ya kifo chake walishangaa kuona wafanyabiashara wa madini wakija katika
msiba na kudai kuwa Prisca alikuwa mfanyabiashara mwenzao, na kuongeza
kuwa marehemu hakuweka wazi kazi yake hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo marehemu alikuwa mfanyabiashara wa madini, mmiliki wa duka la vocha za jumla, duka la vifaa vya ujenzi na mmiliki wa duka la vinywaji maeneo ya Segerea.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo marehemu alikuwa mfanyabiashara wa madini, mmiliki wa duka la vocha za jumla, duka la vifaa vya ujenzi na mmiliki wa duka la vinywaji maeneo ya Segerea.
Marehemu Prisca Paul Rugeiyamu enzi za uhau wake.
Amewaacha yatima watoto watatu, mkubwa ana miaka 12 huku wengine ni
mapacha wana miaka saba. Mwili wa marehemu ulizikwa Januari 15, mwaka
huu katika Makaburi ya Segerea jijini Dar.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.
إرسال تعليق