Wanajamvini,Nawasalimu.
Nimelazimika kuanza na hiyo kauli hapo juu kutokana na unyeti wa habari yenyewe.
Nitakuwa namwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali
yanayoikabili Tanzaniakwa kutumia mifano hai na kumbukumbu rasmi
zilizopo Tanzania.
“Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja
aliye ndani [“Godbless JonathanLema]. Haya maneno aliwahi kuyatoa Mbunge
Lema, nayafananisha na kijitabualichokitoa Mh. January Makamba.
Namheshimu sana [ Hata yeye anajua hilo!]lakini sina budi kusimamia
ukweli na kukemea pale inapobidi!. Tanzania hii iliwahi kupata viongozi
vijana wengi tu lakini historia inaonyesha waliwahi kuligarimu Taifa
kutokana na ufinyu wa kufikiri na uharaka usiokuwa na tija!.Mfano Mh
Raisi Kikwete, ndiye anaonekana kuwa Raisi kijana kuliko wote waliopata
nafasi hiyo kwa siku za usoni lakini makubwa aliyoifanyia taifa hakuna ?
aliwahi kuwa Waziri akiwa na miaka 38 tu?. Hivyo Umri sio kigezo cha
kutushawishi kukupa uongozi. Uraisi sio sawa na kucheza filamu?.
Pili, Vijana tulio wengi hatuitaki ccm, yaani tunayavumilia sana majani
hata hiyo rangi tungeiteketeza kabisa!!!!. Ukiona kijana yupo ccm jua
lazima anapata mnofu? Vinginevyo hakuna au Baba yake aliwahi kuhudumiwa
naccm hivyo na yeye anatega mpira?. Kutokana na sababu hii makini kabisa
tunakuomba sana tena sana [Nakuheshimu sana Mkuu, hata wewe unajua
hilo]usituharibie sifa ya ujana wetu kwa kutaka Makuu wakati bado
unastahili kuwa nasubra baadae kama wataka nafasi hiyo ukaipata [ila
kupitia chama kingine Mkuu].Kutunga kitabu kinachoelezea kuhusu Tanzania
mpya ni maneno tu ambayo kwamtazamo wangu hayana uhalisia wowote ule.
Tatu,Nimewahi kuona watu wengi sana hasa walioko ndani yaccm wakikana
maandiko yao yaliowahi kuwapa PHD, mfano DR. Harrison Mwakembe aliwahi
kuzungumzia muungano wa serikali tatu kwenye kitabu chake lakini baadaye
kupata tu ubunge hatimaye uwaziri kwenye uhalisia akaja kukana maandiko
yake mwenyewe hivyo na hii Tanzania mpya ulioitazamia pindi utakapo
pata nafasi basi itakuwa hivyo hivyo Mkuu , nakushauri egemea kwenye
nini umewahi kuwafanyiaWatanzania na imebaki kama historia nasio
utawafanyia nini tukikupa nafasi [uzoefu ni lulu Mkuu popote pale
Duniani].Mh Nasari aliwahi kusema nanukuu ‘’CCMNI KAMA UKOO WA
PANYA,BABA MWIZI MTOTO MWIZI’’ [Ukikasirika niombee].
Mwisho, Tanzania inahitaji kikongozi mwenye hofu ya Mungu [yaani mwenye
hata kahistoria ka kuwa shehe,padre au hata mchungaji jamani] kutokana
na sababu kuu moja kuwa Tanzania ni nchi pekee Duniani ambayo haina
‘’NationalPolicy’’ mtu akipata nafasi ya uwaziri tu anaweza kusema futa
somo lahesabu kwa shule za msingi watasoma wakiwa sekondari kisa mwanae
halipendi au kwasababu tu ya uswahiba na rafiki yako unaamua tu kuanzia
kesho wewe utakuwa Mkuu wa wilaya [ kwa mfano tu wadau huyo jamaa
alikuwa muuza chipsi leo anapata zali la kuwa mkuu wa wilaya]. Tunataka
kiongozi mwenye hofu ya Mungu ili tutengeneze hizo policy kwanza maana
nchi ipo pabaya.
Ila kiukweli nakupongeza kwa kutangaza nia na sio kwa kutoa kitabu,
tuachie tukupime nini aulichowahi kuifanyi taifa hili Mkuu. Niombee kwa
aliyekasirika. Nawatakia sikunjema
By
Elineema J Mosi
CPA[T]-Arusha,Tanzania.
إرسال تعليق