MREMBO WA FILAMU ANAYECHIPUKIA ASIA MORGAN HATAMPA TALAKA SLIM TALAKA!

MREMBO ambaye aliwahi kunyakuwa Taji la Unique Model, Asia Morgan ambaye pia ni msanii wa filamu anayechipukia, amefunguka kuwa endapo mwigizaji Slim Omary aliyekuwa mumewe hatampa talaka, atampa yeye.


Msanii wa filamu Bongo anayechipukia, Asia Morgan.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Asia ambaye alitengana na Slim akimtuhumu kuwa na wivu wa kupindukia, alisema licha ya kudai talaka mahakamani Slim amekuwa mzito kuitoa hivyo dawa yake ni yeye kumpa.

“Unajua mimi na Slim tusingeachana kwa malumbano kiasi hiki yeye ndiyo chanzo sasa kwa kuwa anagoma kuniandikia takala yangu, nitamuandikia yeye ili tuondoe mzizi wa fitna,” alisema Asia.

Post a Comment

Previous Post Next Post