Msafara wa rais Goodluck wapigwa mawe

Rais Goodluck Jonathan amelaumiwa kwa kukosa kudhibiti kundi la Boko Haram
Msafara wa magari ya Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan umepigwa kwa mawe na watu wanaioishutumu serikali kwa kukosa kukomesha harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Madirisha ya magari kadhaa kwenye msafara huo yalivunjwa kwa mawe, kabla ya polisi kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi watau hao huku wakiwacharaza kwa mijeledi.
Shambulizi hili limefanyika katika mji wa Yola Mashariki mwa Nigeria, ambako Rais Jonathan alikuwa anaendesha kampeni yake kabla ya uchaguzi mkuu mwezi ujao.
Maelfu ya wakimbizi wa ndani wanaishi mjini Yola baada ya kutoroka vita kutoka makwao ambako Boko Haram inaendesha harakati zake.(BBC)

Post a Comment

Previous Post Next Post