Msafara
wa magari ya Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan umepigwa kwa mawe na
watu wanaioishutumu serikali kwa kukosa kukomesha harakati za wapiganaji
wa kiisilamu wa Boko Haram.
Madirisha ya magari kadhaa kwenye
msafara huo yalivunjwa kwa mawe, kabla ya polisi kuwafyatulia gesi ya
kutoa machozi watau hao huku wakiwacharaza kwa mijeledi.
Shambulizi
hili limefanyika katika mji wa Yola Mashariki mwa Nigeria, ambako Rais
Jonathan alikuwa anaendesha kampeni yake kabla ya uchaguzi mkuu mwezi
ujao.
Maelfu ya wakimbizi wa ndani wanaishi mjini Yola baada ya
kutoroka vita kutoka makwao ambako Boko Haram inaendesha harakati zake.(BBC)
إرسال تعليق