Muimbaji wa Uganda, Juliana Kanyomozi amefunguka kwa urefu kuhusiana na masuala mbalimbali kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa SatisfashionUG.
Miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni pamoja na kuvuja kwa picha za utupu
za muimbaji mwenzie wa Uganda, Desire Luzinda. “Kwanza kabisa katika
kesi nyingi kamwe huwa sio kosa la mwanamke,” anasema Juliana.
“Kama wewe ni mtu mzima na umempenda mtu unajua kuwa hakuna kikomo
cha kipi kitatokea kwenye chumba binafsi cha watu wazima wawili. Kama
hautaenda mbali zaidi kumfurahisha mwanaume wako, atakuacha na kisha
utahukumiwa kwa hilo,” aliongeza.
“Pindi mwanaume anapovunja uaminifu na kuamua kushare vitu hivyo siri
kwa dunia nzima na kutumia vyote dhidi ya mwanamke – ndio maana bado
tuna safari ndefu kama wanawake kukemea tabia hiyo.”
“Nachukizwa na wanaume wa aina hii. Wanatia aibu. Kinachoshangaza
zaidi ni kuwa ni wanawake pekee ndio wanaokuwa wahanga kwenye visasi
hivi vya mashambulizi ya purn. Unapofanya kitu kama hicho kwa mwanamke,
hauwaumizi wanawake wote tu bali pia mama yako, mabinti zako na dada
zako.”
Juliana alitolea pia mfano wa udukuzi uliofanyika nchini Marekani na
kudai kuwa pamoja na picha za wasanii mbalimbali kuvuja hakuna chombo
cha habari cha kuaminika kilichozianika.
“Inanisikitisha hapa nyumbani, kinyume chake ndio kinatokea."
إرسال تعليق