Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ akimlisha keki rafiki yake, 'wastara'.
Na Hamida Hassan/Ijumaa Staa wa filamu za Kibongo,
Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alifanyiwa pati ya bethidei ambapo
kwenye zoezi la kuwalisha keki mashosti zake, aliwashangaza watu kwa
kusema wote atawalisha kwa mdomo ‘staili ya kudendeka’.
‘Amanda’akiwalisha keki mashosti zake.
Pati hiyo ilifanyika juzikati kwenye Ukumbi wa Tamigamiga, Mbezi
Beach jijini Dar ambapo mbali na staili hiyo ya kulishana keki, eneo la
tukio lilitawaliwa na vituko kutokana na mastaa wengi kuwa bwii.
‘Amanda’akipozi na mdogo wake anayefahamika kwa jina la Sabrina.
Akizungumzia sherehe hiyo Amanda alisema: “Ilikuwa ni siku muhimu
sana kwangu na nilifarijika kuona wasanii wengi kama vile Riyama, Esha
Buheti, Wastara na wengineo wamejitokeza kufurahi na mimi. Ila kulishana
keki vile ni staili ya kinjiwanjiwa, hahaaa!”
إرسال تعليق