Serikali: hatujaapisha viongozi Migombani

DaresSalaam. Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali  kuapishwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi, akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.
Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili kama inavyozaniwa.
“Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au kamishna wa viapo,” alisema Kidera na kuongeza kuwa:
“Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea.”

Post a Comment

Previous Post Next Post