DaresSalaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali kuapishwa kwa
mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi,
akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu
wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa
mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya
kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.
Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo,
mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la
Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea
kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani
kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili
kama inavyozaniwa.
“Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani
badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha
viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi
wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria
zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au
kamishna wa viapo,” alisema Kidera na kuongeza kuwa:
“Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza
baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi
nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na
wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea.”
إرسال تعليق