Benki ya Dunia yatoa viwango vya ukuaji uchumi

Mkuu wa Uchumi wa Benki ya Dunia Olivier Blanchard akiongea na wanahabari Beijing, China, Jumanne, Januari, 20, 2015.
Benki ya dunia imetoa matarajio yake ya kiuchumi kwa mwaka 2015, na kusema uchumi wa dunia unakabiliana na kile mkuu wake alichokiita “mawimbi makubwa na magumu.”
Benki ya Dunia bado inatarajia ukuwaji wa asilimia 3.5 kwa mwaka huu wa 2015 na asilimia 3.7 kwa mwaka ujao wa 2016.
Pamoja na ukuaji huo viwango vyote vipo chini kwa tatu ya kumi kutoka katika matarajio ya benki hiyo ya mwezi Oktoba, mwaka jana.
Mchumi mkuu wa Benki ya Dunia, Oliver Blanchard, amewaambia wanahabari Jumanne mjini Beijing, China, kwamba uchumi wa dunia unatarajiwa kukuwa kwa kiasi kwa mwaka huu wa 2015.
Ukuaju huo ni zaidi ya ukuaji wa mwaka jana,  licha ya matazamio ya ukuaji hafifu wa kiuchumi kwa sehemu kubwa ya dunia.
- V.A

Post a Comment

أحدث أقدم