DEREVA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI ALILOKUWA AKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA WILAYANI MBOZI.
DEREVA ALIYEKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.910 CVF AINA YA TOYOTA NOAH ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA STANFORD LUENJE (30) MKAZI WA MBOZI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI HILO KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO ENEO LA MLOWO WILAYANI MBOZI.

TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:30 HUKO ENEO LA
MLOWO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA
KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NDIMYAKE
MWAKISU (33) NA 2. ELISHA MWASHUYA (30) WOTE WAKAZI WA MBOZI
WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI KWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N.
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
إرسال تعليق