Tambua vipashio vya kiima na kiarifu katika sentensi

Katika aina za vishazi kuna vishazi tegemezi vivumishi. Hivi hujitokeza katika mazingira yafuatayo katika tungo:
Vishazi tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwa. Pia vishazi tegemezi visivyoambatana na nomino inayovumishwa.
Aina nyingine ni vishazi tegemezi vielezi ambavyo huwa vishazi tegemezi vya mahali, vya wakati, vya namna au jinsi vya masharti, vya hali, hitilafu au kasoro iliyoko katika tendo na vya chanzo au sababu.
Vishazi vinaweza kuwa na dhima na hadhi ili uweze kubaini kwa urahisi. Kishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kwa kuwa na maana kamili inayojitosheleza.
Hata hivyo, kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali hutegemea vishazi vingine.
Mfano; Aliyekwenda shule jana...(kishazi tegemezi)
Hata hivyo, Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili).
Mfano; Aliyekwenda jana...amerudishwa kwa kukosa ada. (kishazi huru japokuwa kuna kiima kapa kinachohitaji kubainishwa ni nani anayetajwa).
Kishazi tegemezi hakina hadhi hii, vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi vingine hushuka daraja na kuchukua dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi hufanya kazi ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.
Mfano; Mwanafunzi aliyechapwa sana. ‘Aliyechapwa sana’ imesimama kama kishazi kinachovumisha nomino ya ‘mwanafunzi’, ila bado ni kishazi tegemezi kwa kuwa hakuna taarifa kamili kuhusu mwanafunzi aliyechapwa sana, je, nini kimefuata au kimetokea.
Tujadili kiwango kingine cha tungo ambacho ni sentesi. Kumbuka tulianza kwa kuelezea tungo neno, tungo kirai, tungo kishazi, sasa ni tungo sentensi.
Sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na kinacholeta maana kamili.
- Soma Zaidi Hapa

Post a Comment

Previous Post Next Post