Mwandishi
Mike Keegan wa Daily Mail, anaongeza idadi ya waandishi na wachambuzi
wa soka wanaohoji mbinu za kocha wa Manchester United Louis van Gaal.
Hakuna
mchambuzi wa soka nchini England anayekubaliana na mfumo wa 3-5-3
unaotumiwa na Van Gaal na sasa Mike Keegan anashangaa ni vipi kiungo
aliyesajiliwa kwa bei mbaya Angel Di Maria achezeshwe kama mshambuliaji.
Mike anasema wakati Di Maria akisajiliwa kwa pauni milioni 59.7, Van Gaal akasema amempata mmoja wa wachezaji bora duniani.
Lakini Di Maria aliyepewa jezi namba 7 iliyotumiwa na wakali kama Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo, bado hatumiki vizuri United.
Mwandishi
huyo anashangaa ni vipi Di Maria achezeshwe kama mshambuliji badala ya
kiungo wa pembeni halafu hapo hapo unamrudisha mshambuliaji Wayne Rooney
akacheze nafasi ya kiungo.
Kama
vile hiyo haitoshi, Mike anahoji ni vipi beki Phil Jones anapata nafasi
ya kupiga kona mbele ya Rooney, Di Maria na Juan Mata. Van Gaal anajua
anachofanya? Anahoji mwandishi huyo.
Mike
Keegan alikuwa akichambua mechi ya QPR na Manchester United ambapo
alisema kipindi cha pili hususan baada ya Van Gaal kubadili mfumo na
kucheza 4-4-2, kilikuwa na msismiko zaidi na hakushangaa United
ilipopata magoli mawili na kuchukua pointi tatu muhimu.
Anasema hakubaliani na usemi wa Van Gaal ya kwamba anapochezesha mfumo wa 4-4-2 timu inakosa uwiano.
Aidha mwandishi huyo amewashutumu mabeki Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans kwa kushindwa kufunika mapengo ya Nemanja Vidic, Patrice Evra na Rio Ferdinand.
إرسال تعليق