SAKATA la wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24)
mkazi wa Stakishari, Ukonga, Dar es Salaam na Lucy Fred (23) mkazi wa
Karakata, Dar ambao walishikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari,
Ukonga jijini kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja limechukua
sura mpya.
Habari za kipolisi zinasema wasichana hao ambao walifunguliwa jalada
kituoni hapo namba SKT/RB/463/2015 baada ya kukamatwa Januari 12, mwaka
huu inadaiwa kuwa walioana.
“Zipo picha zinazodaiwa kuwa walioana na wanaonekana wakiwa
wanavishana pete nyingine wakiwa wanafungua shampeni kwenye hafla fupi
ambayo waliifanya jijini Dar es Salaam,” kilisema chanzo ndani ya jeshi
la polisi.
Habari zaidi zinadai kuwa hafla hiyo waliifanyia katika ukumbi mmoja
(jina tunalihifadhi) ambao upo Chang’ombe na unatumika kwa shughuli
nyingi za burudani na hata michezo.“Mimi nilihudhuria sherehe hiyo na
picha ninazo ambazo zinawaonesha wasichana hao wakivishana pete na
walikuwepo pia waalikwa kama unavyoona kwenye sherehe za harusi katika
jamii yetu,” alisema mtu mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi.
Mtu huyo alidai kuwa mmoja wa wasichana hao anamfahamu kwa kuwa sasa
hivi anaishi kwa dada yake karibu na Uwanja wa Ndege, Karakata nyuma ya
msikiti mpya.Mara baada ya kukamatwa wasichana hao, Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Mogo, Stakishari,George Mtambalike alilithibitishia
gazeti hili ofisini kwake kutiwa mbaroni kwao kwa madai ya kufanya
mapenzi ya jinsia moja.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki
alisema wasichana hao bado wanapelelezwa. “Ni kwamba kesi yao ipo
Stakishari na uchunguzi dhidi yao ukikamilika watafikishwa mahakamani, “
alisema Kamanda Nzuki.

إرسال تعليق