Wanawake arobaini na tano wamepoteza maisha wakati wa kujifungua
katika hospitali ya wilaya ya manyoni kwa kipindi cha mwaka elfu mbili
na kumi na mbili hadi elfu mbili na kumi na tatu kwa sababu
mbalimbabali.
Mratibu wa afya ya mama na mtoto wa halmashauri ya wilaya ya
manyoni, Bi. Hapiness Mazala amesema hayo alipokuwa akieleza ITV hali
halisi ya vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua
vilivyotokea katika kipindi cha miaka mitatu.
Bi. Hapiness amesema kati ya akina mama hao arobaini na tano
waliopoteza maisha wakati wa kujifungua ,kumina tano kati yao
walipoteza maisha yao mwaka elfumbili na kumina mbili,wakati kwa mwaka
eilfu mbili na kumina tatu akina mama kumina sita na mwaka elfumbili
na kumina nne ni akina mama kumina nne walipoteza maisha.
Hata hivyo alifafanua pia kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka
elfumbili na kumina mbili hadi mwaka elfu mbili na kumina nne jumla ya
akina mama miamoja na sita walipatiwa huduma za kujifungua kutoka kwa
wakunga wa jadi,ambapo kati yao thelasini na tano walijifungua mwaka
elfu mbili na kumina tatu na mwaka jana ni akina mama sabini na moja
walijifungulia kwa wakunga hao wa jadi.
Kwa mujibu wa madhara kati ya wakunga wa jadi miamoja arobaini
nanne na waganga wa jadi mianne sitini na nne waliopo katika wilaya
ya manyoni ,waliosajiliwa ni wakunga kumi tu na waganga wa jadi
waliosajili ni miamoja hamsini nanane , jambo ambalo ni hatari
kwasababu baadhi ya wanganga wa jadi na wakunga wa jadi ina kuwa vigumu
kuwapata pindi matatizo yanapo tokea wakati wa kutoa huduma zao.
Post a Comment