Mvutano wa mgogoro wa wakulima na halmashauri ya wilaya wachukua sura mpya Kilimanjaro

Wakulima wa kikundi cha mbuyuni wilaya ya hai waeiomba serikali mkoani kilimanjaro  iingilie kati mgogoro kati yao na halmashauri ya wilaya hiyo ambayo inataka kuwapora jengo lao kwa mabavu ambalo waliilazima serikali ya kijiji cha bomang'ombe bila  bila malipo kuanzia mwaka 1976.
Mwenyekiti wa kwanza wa kikundi hicho Bw Seleman Mmbwambo amesema, waliamua kuiazima bure serikali ya kijiji hicho baada ya kukosa ofisi ili iweze kuwahudumia wananchi katika mazingira mazuri.
Bw Mmbwambo amesema, walipohitaji warejeshewe jengo hilo kwa matumizi yao mengine halmashauri hiyo  ilikataa na wakaamua kulipeleka suala hilo mahakama ya ardhi ya moshi   ambayo iliwapa ushindi na kuiagiza halmashauri ihame katika jengo hilo ambalo sasa ni ofisi za kata ya hai mjini tarafa .
Aliyekuwa afisa mtendaji wa kijiji hicho kati wakati huo Bw  Mohamed Kasimu amethibitisha uhalali wa wakulimma hao kuwa wamiliki halali wa jengo hilo kwa mujibu wa nyaraka zilizopo na halmashauri ya wilaya inalazimisha kuwapora wakulima mali yao.
Katibu wa sasa wa kikundi hicho Bw Rasuli Mohamed  amesema, zipo kumbukummbu za barua ambazo zinaonyesha maombi ya serikali ya kijiji ya kuomba kuazima jengo hilo kutoka kwao lakini wanaishangaa halmashauri hiyo kutaka kuwadhulumu wakulima hao jasho lao.
Dalali wa mahakama ya ardhi ya wilaya ya hai aliyepewa jukumu la kulikabidhi jengo hilo kwa wakulima hao Bw  Hamadi Ramadhani ameishtumu halmashauri hiyo kuling'ang'ania jengo hilo huku akijua si mali yao.
Mwenyekiti wa baraza la ardhi la moshi Mhe Musa Mahelele amethibitisha kukipa ushindi kikundi hicho baada ya halmashauri hiyo kushindwa kufika mbele ya baraza kwa muda mrefu na ilipoingilia kati halm hiyo ilishauriwa ifungue upya kesi kupinga uamuzi huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post