Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza
kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa
tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa pili kulia), wakimsikiliza mmoja wa
wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO (haonekani pichani) wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara
ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mmoja wa
wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya.
Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt.
Mighanda J. Manyahi (wa sita kutoka kushoto) wakimsikiliza Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng.Ngosi Mwihava (wa tano kulia) mara
baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Wajumbe wengine wa Bodi hiyo
(kutoka kushoto) ni Dkt. Nyamajeje C. Weggoro, Eng. Boniface C. Muhegi,
Dkt. Mutesigwa I. Maingu, Bw. Shaaban S. Kayungilo, na Dkt. Haji H.
Semboja. Wajumbe wengine (kutoka kulia) ni Bibi. Kissa Vivian Kilindu,
Bw. Felix G. Kibodya na Eng. Juma F. Mkobya.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
akiwapongeza Wajumbe wa Bodi mpya ya TANESCO mara baada ya kuizindua
Bodi hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa vipaumbele vya utekelezaji wa
majukumu. Wanaoshuhudia ni viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini
wakiongozwa na Naibu Waziri, Stephen Masele (kushoto kwa Waziri) na
Kaimu Katibu Mkuu, Eng. Ngosi Mwihava (wa nne kulia).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza
kushoto) akisisitiza jambo mara baada ya kuzindua Bodi mpya ya TANESCO
katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa
tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne
kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi
Mramba (wa nne kulia). Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo,
Eng. Juma Mkobya,(wa tatu kulia), Bw. Felix G. Kibodya (wa pili kulia),
Bibi. Kissa Vivian Kilindu (wa kwanza kulia), pamoja na watendaji
mbalimbali wa TANESCO (waliokaa mstari wa nyuma).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Mighanda J.
Manyahi (aliyesimama) akizungumza mara baada ya Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es
Salaam. Wanaomsikiliza ni Waziri, Profesa Muhongo (kulia) na Mjumbe wa
Bodi hiyo, Dkt. Haji H. Semboja (kushoto). Picha kwa hisani ya Mdimuz
Blog
Post a Comment