Waziri wa Nishati na Madini azindua Bodi mpya ya Tanesco

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa pili kulia), wakimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO (haonekani pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya.
Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Mighanda J. Manyahi (wa sita kutoka kushoto) wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng.Ngosi Mwihava (wa tano kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Wajumbe wengine wa Bodi hiyo (kutoka kushoto) ni Dkt. Nyamajeje C. Weggoro, Eng. Boniface C. Muhegi, Dkt. Mutesigwa I. Maingu, Bw. Shaaban S. Kayungilo, na Dkt. Haji H. Semboja. Wajumbe wengine (kutoka kulia) ni Bibi. Kissa Vivian Kilindu, Bw. Felix G. Kibodya na Eng. Juma F. Mkobya.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwapongeza Wajumbe wa Bodi mpya ya TANESCO mara baada ya kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu. Wanaoshuhudia ni viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Naibu Waziri, Stephen Masele (kushoto kwa Waziri) na Kaimu Katibu Mkuu, Eng. Ngosi Mwihava (wa nne kulia).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo mara baada ya kuzindua Bodi mpya ya TANESCO katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa nne kulia). Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya,(wa tatu kulia), Bw. Felix G. Kibodya (wa pili kulia), Bibi. Kissa Vivian Kilindu (wa kwanza kulia), pamoja na watendaji mbalimbali wa TANESCO (waliokaa mstari wa nyuma).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Mighanda J. Manyahi (aliyesimama) akizungumza mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Waziri, Profesa Muhongo (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt. Haji H. Semboja (kushoto). Picha kwa hisani ya Mdimuz Blog

Post a Comment

أحدث أقدم