Wakulima wa kikundi cha mbuyuni
wilaya ya hai waeiomba serikali mkoani kilimanjaro iingilie kati
mgogoro kati yao na halmashauri ya wilaya hiyo ambayo inataka kuwapora
jengo lao kwa mabavu ambalo waliilazima serikali ya kijiji cha
bomang'ombe bila bila malipo kuanzia mwaka 1976.
Mwenyekiti wa kwanza wa kikundi hicho Bw Seleman Mmbwambo amesema,
waliamua kuiazima bure serikali ya kijiji hicho baada ya kukosa ofisi
ili iweze kuwahudumia wananchi katika mazingira mazuri.
Bw Mmbwambo amesema, walipohitaji warejeshewe jengo hilo kwa
matumizi yao mengine halmashauri hiyo ilikataa na wakaamua kulipeleka
suala hilo mahakama ya ardhi ya moshi ambayo iliwapa ushindi na
kuiagiza halmashauri ihame katika jengo hilo ambalo sasa ni ofisi za
kata ya hai mjini tarafa .
Aliyekuwa afisa mtendaji wa kijiji hicho kati wakati huo Bw
Mohamed Kasimu amethibitisha uhalali wa wakulimma hao kuwa wamiliki
halali wa jengo hilo kwa mujibu wa nyaraka zilizopo na halmashauri ya
wilaya inalazimisha kuwapora wakulima mali yao.
Katibu wa sasa wa kikundi hicho Bw Rasuli Mohamed amesema, zipo
kumbukummbu za barua ambazo zinaonyesha maombi ya serikali ya kijiji ya
kuomba kuazima jengo hilo kutoka kwao lakini wanaishangaa halmashauri
hiyo kutaka kuwadhulumu wakulima hao jasho lao.
Dalali wa mahakama ya ardhi ya wilaya ya hai aliyepewa jukumu la
kulikabidhi jengo hilo kwa wakulima hao Bw Hamadi Ramadhani ameishtumu
halmashauri hiyo kuling'ang'ania jengo hilo huku akijua si mali yao.
Mwenyekiti wa baraza la ardhi la moshi Mhe Musa Mahelele
amethibitisha kukipa ushindi kikundi hicho baada ya halmashauri hiyo
kushindwa kufika mbele ya baraza kwa muda mrefu na ilipoingilia kati
halm hiyo ilishauriwa ifungue upya kesi kupinga uamuzi huo.
إرسال تعليق