Ngorongoro. Polisi wilayani Ngorongoro, Mkoa wa
Arusha, inawashikilia wafugaji wawili kwa kosa la kukutwa na bunduki
aina ya Rifle wanayodaiwa kuitumia kufanya uhalifu wilayani hapa na
Kenya.
Katika msako ulioongozwa na Mkuu wa Polisi wa
wilaya hiyo, Mrakibu (SP), Ally Mohamed Mkalipa alisema walifanikiwa
kukamata silaha hiyo iliyokuwa imefichwa porini karibu na boma la
ng’ombe la mfugaji mmoja.
Akizungumza jana na gazeti hili, Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Liberatus Sabas
aliwataja wafugaji hao kuwa ni wakazi wa Kijiji cha Soitisambu.
Kamanda Sabas alitaja silaha hiyo ni Rifle 370 na
tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu saa 11 jioni katika Kitongoji
cha Silalei, Kijiji cha Soitisambu, Loliondo
إرسال تعليق