SASA
ni rasmi kwamba kazi ya kuliboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura
nchini kote, itaanza Jumatatu ijayo Februari 16 na kumalizika Aprili 29
mwaka huu.
Pinda
alimtoa wasiwasi Mbowe kuhusu ufanisi wa vifaa hivyo vya BVR, kwa
kusema endapo tume itaona kuwa uandikishaji huo hauwezekani kwa sababu
yoyote ile, itatoa taarifa bungeni na serikali iko tayari kubadili
maamuzi
Uandikishaji huo utaanzia katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mtwara na Njombe na baadaye utahamia katika mikoa mingine.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema ratiba ya upigaji wa kura ya maoni
ambayo ni Aprili 30 iko pale pale, kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya
Kikwete. Wakati uandikishaji huo ukianzia katika mikoa minne, utafungwa
kwa kumalizia Dar es Salaam na Zanzibar.
Akizungumza
jana ofisini kwake, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura na Habari wa
NEC, Ruth Masham aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika
uboreshaji wa daftari la wapigakura baada ya utoaji wa elimu kwa
waratibu kukamilika.
Alisema
tume hiyo imetoa elimu kwa waratibu wa waandikishaji kwa kila mkoa na
katika kila mkoa wametoa mafunzo hayo kwa mratibu mmoja.
Pia,
elimu imetolewa kwa maofisa waandikishaji wa Halmashauri, na wasaidizi
wao na hao ndio watakaotumika kutoa elimu kwa waandikishaji wadogo
katika ngazi za tarafa na kata.
Masham
alisema ni haki ya kila Mtanzania kujiandikisha. Alisema wananchi wana
haki ya kutumia fursa hiyo ya kujiandikisha ili ifikapo Oktoba mwaka huu
waweze kutumia haki hiyo ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka.
“Kila
Mtanzania atapata fursa ya kujiandikisha na kupata kitambulisho chake
ambacho atakitumia wakati wa kupiga kura. Hivyo tunawaasa watanzania
wote wanaposikia uboreshaji umefika katika eneo lake ajitokeze
kujiandikisha,” alisema.
Katika
kikao cha Bunge kilichomalizika wiki iliyopita, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda aliwahakikishia Watanzania kuwa uandikishwaji wa wapiga kura ambao
utatumia Mfumo wa Kielektroniki (BVR), utafanyika kwa ufanisi na kwa
wakati uliopangwa.
Akijibu
swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
kuhusu uhakika wa uandikishaji huo, Pinda alisema tume ya uchaguzi
inaamini kuwa vifaa vitakavyotumika, vina ubora mara mbili ya
vilivyoletwa kwa ajili ya uandikishaji wa majaribio.
Licha
ya kukiri kuwa awali serikali ilikuwa na tatizo la kifedha, Pinda
alisema tume imewahakikishia kuwa shughuli zote za upigaji kura kwa
ajili ya Katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu, zitafanyika.
Post a Comment