NGULI
wa filamu za Kibongo, Davina Yahaya ‘Davina’, amesema kamwe hatokuja
kusahau mateso aliyowahi kuyapata akiwa Gereza la Segerea ambapo alikaa
kwa siku tatu.
Nguli wa filamu za Kibongo, Davina Yahaya ‘Davina’.
Akipiga stori na Uwazi, Davina alisema tukio hilo lilitokea mwishoni
mwa mwaka 2012 ambapo ilikuwa ni tatizo la kifamilia lililosababisha
kutupiwa huko japokuwa hakuweza kuliweka hadharani kwakuwa bado lipo
mikononi mwa sheria.
“Huwa natokwa machozi na kamwe sitokuja kusahau mateso niliyoyapata
Segerea. Nilikuwa kwa siku tatu lakini niliona kama mwezi, hali ya hewa,
sehemu ya kulala zilikuwa mbaya sana, wingi wa watu na sikupata hata
nafasi ya kulala zaidi ya kukesha nikilia,” alisema Davina.
Post a Comment