Hatima
ya kiongozi wa upinzani nchini Malaysia Anwar Ibrahim ni mwezi march
mwaka huu iwapo atafungwa jela ama kuwa huru dhidi ya mashtaka yake ya
ulawiti.
Mahakama kuu ya Malaysia inatarajiwa kupitia rufani ya
Anwar aliyekutwa kutwa na makosa ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na
msaidizi wake wa kiume mwaka 2008.
Hata hivyo Anwar mwenyewe
anasema kuwa mashtaka haya dhidi yake ni sehemu ya kampeni za kisiasa
kutaka kumpunguzia hadi yake zinazofanywa na chama tawala cha UMNO.
Anwar
aliyekuwa naibu waziri mkuu wa Malaysia miaka ya 90 alijiunga na
upinzani,na alifungwa jela kwa miaka sita baada ya kubainika na makosa
ya ufisadi na mapenzi ya jinsia moja kabla ya mashtaka mengine kama hayo
yaliyomkumba kwa mara ya pili.(BBC)
Post a Comment