Profesa Anna Tibaijuka
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rebecca Mngodo, alimtaka Tibaijuka atumie bilioni 1.6 alizopata katika mgawo wa Escrow kusaidia awamu ya pili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera ambao umekwama.
Mngodo alisema hayo wakati akichangia mjadala kuhusu taarifa za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na ya Nishati na Madini.
"Tibaijuka angekuwapo hapa, zile bilioni 1.6 angesaidia kulipa," alishauri Mngodo.
Profesa Tibaijuka alikaririwa akithibitisha kupata mgawo wa fedha hizo kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering & Marketing, James Rugemalira, kumsaidia kuendeleza shule ya Babro Johansson iliyoko Kwembe Dar es Salaam.
Kutokana na kitendo hicho, Rais Jakaya Kikwete, alimfukuza kazi Tibaijuka kutokana na kukiuka maadili ya uongozi yasiyoruhusu kupokea zawadi kwa kificho.
Post a Comment