STAA
wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa kali ya aina yake
baada ya kusema anavutiwa na taasisi huru ya imani ya Freemason kutokana
na umakini mkubwa walionao kwenye kazi zao. Akipiga stori na paparazi
wetu, Baby alisema watu wengi wamekuwa wakizungumza kwa mitazamo tofauti
kuhusiana na Freemason lakini kiuhalisia, watu wa imani hiyo ni makini
wanaojitambua na kujiheshimu.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akipozi.
“Hawa jamaa kiukweli siyo wa kuchezewa kabisa, lakini ukweli tu ni
kwamba nawazimikia mno na ndiyo sababu mara nyingi hata ukiangalia kazi
zangu za muziki utakutana na nembo zao kivyovyote vile, sema siwezi
kujiunga nao,” alisema Baby Madaha.
إرسال تعليق