SUZY RAHA YA MWANAUME ADEKE!

MSANII wa kitambo katika anga la filamu Bongo, Happy Nyatawe ‘Suzy’ amesema katika suala la uhusiano siku zote anampenda mwanaume anayejua kudeka.
Msanii wa kitambo katika anga la filamu Bongo, Happy Nyatawe ‘Suzy’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Suzy alisema mwanaume anayejua kujidekeza ndiye mzuri lakini ambaye anajidai ni mgumu na kuleta masharti yeye siyo fani yake kabisa.
“Mwanaume mwenye masharti kama ugonjwa wa kisukari simtaki, mwanaume anayedeka ndiyo mpango mzima, halafu anayependa kuvaa kanzu hapo ndiyo atanimaliza kabisa,” alisema Suzy.

Post a Comment

أحدث أقدم