VIBAKA WANUSURIKA KUUAWA KWA KIPIGO JIJINI MWANZA LEO


Vijana hao baada ya kula kichapo kutoka kwa wananchi.
Wananchi wa eneo la Deluxe baada ya kuwapa kichapo cha kutosha vibaka hao.
Wananchi wenye hasira kali wakiwa wamewazingira vibaka hao.
 
Vibaka hao wakipakizwa kwenye difenda ya polisi.
 
Vibaka hoi ndani ya difenda.
 
Polisi wakiondoka na vibaka hao kwenye difenda.
Na Waandishi Wetu, Mwanza
VIJANA wawili wanaosadikiwa kuwa ni vibaka wamekumbana na kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika Mtaa wa Deluxe jijini Mwanza majira ya saa 5:30  leo asubuhi wakituhumiwa kwa wizi wa kofia kutoka duka moja lililopo maeneo hayo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, vijana hao ambao majina yao hayakuweza kufahamika waliingia katika duka hilo kama wateja na kuulizia vitu mbalimbali katika duka hilo na baadaye kuwazunguka wauzaji wa duka na kuchukua kofia aina ya kapero kitu kilichopelekea kupigiwa kelele za wezi ndipo walipoanza kushushia kichapo.
Matukio kama haya ya vibaka kuvamia na kuchukua vitu katika maduka na kwa watu yamekuwa yakitokea mara kwa mara jijini hapa na mara nyingi wahusika wamekuwa wakipata vichapo vya kutosha japo wamekuwa wakiokolewa na Jeshi la Polisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post