Vijana hao baada ya kula kichapo kutoka kwa wananchi.
Wananchi wa eneo la Deluxe baada ya kuwapa kichapo cha kutosha vibaka hao.
Wananchi wenye hasira kali wakiwa wamewazingira vibaka hao.
Vibaka hao wakipakizwa kwenye difenda ya polisi.
Vibaka hoi ndani ya difenda.
Polisi wakiondoka na vibaka hao kwenye difenda.
Na Waandishi Wetu, Mwanza
VIJANA wawili wanaosadikiwa kuwa ni vibaka wamekumbana na kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika Mtaa wa Deluxe jijini Mwanza majira ya saa 5:30 leo asubuhi wakituhumiwa kwa wizi wa kofia kutoka duka moja lililopo maeneo hayo.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, vijana hao ambao majina yao
hayakuweza kufahamika waliingia katika duka hilo kama wateja na kuulizia
vitu mbalimbali katika duka hilo na baadaye kuwazunguka wauzaji wa duka
na kuchukua kofia aina ya kapero kitu kilichopelekea kupigiwa kelele za
wezi ndipo walipoanza kushushia kichapo.
Matukio kama haya ya vibaka kuvamia na
kuchukua vitu katika maduka na kwa watu yamekuwa yakitokea mara kwa mara
jijini hapa na mara nyingi wahusika wamekuwa wakipata vichapo vya
kutosha japo wamekuwa wakiokolewa na Jeshi la Polisi.
إرسال تعليق