WILFRIED BONY AIPELEKA IVORY COAST NUSU FAINALI, ALGERIA YAFA 3-1

Hatimaye Wilfried Bony ameondoa ukame wake wa magoli kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuifungia Ivory Coast mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Algeria.
Kabla ya hapo, Bony aliyesajiliwa na Manchester City hivi karibuni na kuwa mchezaji ghali zaidi Afrika, alikuwa hajafunga hata goli moja kwenye michuano hii.
Mshambuliaji huyo alifunga bao la kwanza dakika ya 24 lakini El Arabi Soudani akaisawazishia Algeria mwanzoni tu mwa kipindi cha pili.
Wilfried Bony akaongeza bao la pili baada ya kuunganisha free-kick ya Yaya Toure kabla ya Gervinho kufunga la tatu katika dakika za majeruhi.
Ivory Coast: Gbohouo, Aurier, Bailly, Toure, Kanon, Tiene (Diomande 67), Gradel, Toure, Serey Die, Gervinho, Bony (Tallo 90)

Algeria: M'Bolhi, Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Taïder, Bentaleb, Feghouli, Brahimi, Mahrez (Slimani 72 mins), Soudani (Belfodil 72)

Post a Comment

أحدث أقدم