Chamwino. Zaidi ya Sh5.9 milioni zilizodaiwa
kimeibwa na baadhi ya maofisa watendaji wa kata na vijiji katika
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma zimerejeshwa.
Fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa maabara za shule za sekondari wilayani hapa.
Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Ally alisema hayo hivi
karibuni wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo katika Kikao
cha Baraza la Madiwani.
Alisema fedha hizo zimerudishwa kutoka kwa watendaji wanane wa kata na vijiji.
Alizitaja kata hizo kuwa ni Fufu, Handali, Mlowa Bwawani, Haneti Chilonwa, Manda, Chinungulu na kijiji cha Chifukulo.
Alisema watendaji hao walingundulika kuchukua
fedha hizo baada ya kukaguliwa vitabu vyao vya kuchangisha michango toka
kwa wananchi.
Alisema watendaji hao baada ya kurudisha fedha
hizo hatua walizochukuliwa ni pamoja na kupewa onyo kali ikiwa na
kuangaliwa katika utendaji wao kwenye maeneo ya vituo vya kazi.
Pia, alisema walikamatwa na kufikishwa Kituo cha
Polisi cha Chamwino Ikulu na kufunguliwa shtaka la kesi ya wizi wa fedha
zilizochangwa na wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Saada
Mwaluka aliwataka watendaji wa vijiji na kata kutoa orodha ya majina ya
wananchi wanaochangia ujenzi wa maabara na kuyabandika kwenye ofisi za
vijiji na vitongoji ili kuwabaini wasiochangia.
Pia, aliwataka kusoma mapato na matumizi kwenye mikutano ya hadhara kwa wakati kama sheria na taratibu zinavyoelekeza
- Mwananchi
Post a Comment