Viongozi
mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye
Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim
Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi
kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam
leo.
Maelfu ya
waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia
Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro,
Kariakoo na tayari kwa kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele,
Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya
Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiongoza shughuli
ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim
Mbita kuelekea kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini
Dar es Salaam leo
إرسال تعليق