Timu ya klabu ya Yanga imeondoka nchini
usiku wa kuamkia leo kuelekea nchini Tunisia kucheza pambano la marudiano dhidi
ya Etoile huku ikimwacha kiungo wake tegemezi Haruna
Hakizimana Fadhil Niyonzima ambaye ni majeruhi.
Niyonzima hawezi kabisa kwenda kucheza kwa sababu bado hajapona
kabisa.
Kikosi cha Yanga kilichoenda Tunisia ni hiki,
makipa
Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’,
Mabeki
Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
Viungo
Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma
‘Makapu’, wakati
washambuliaji
Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman,
Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva.
Yanga SC inahitaji
ushindi wa ugenini au sare kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya
kufungana bao 1-1 na Etoile katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki
iliyopita.
إرسال تعليق