MAAJABU YA MWAKA DAR!

HII kali! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Alice May John (55) ameilalamikia nyumba yake iliyopo Sinza ‘D’ (Madukani) wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam kwamba, ina mauzauza ya kutisha, hali inayowafanya wapangaji kuikimbia kila wakati kwa kuhofia maisha yao.

Alice May John anayelalamikia nyumba yake iliyopo Sinza ‘D’ (Madukani) kuwa na mauzauza.
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni nyumbani kwake, Alice alisema amekuwa akibanwa na wapangaji awarudishie kodi zao ili watafute nyumba nyingine kutokana na kelele zinazosadikiwa ni za binadamu lakini hawaonekani.
...wakiwa nje ya nyumba hiyo na mwandishi wa Global Publishers.
“Wakati nahamia hapa mwaka 2004 kutokea Mabibo (Dar) nilikorofishana na mzee mmoja akanitishia maisha kwa kuniambia nitaona na ndipo majitu hayo yakaanza kupiga kelele ya kulia usiku au mchana, wanalia hiiiii, hiiii, hiiii! Unaweza kusikia kutokea chumbani, ukiingia huoni mtu.
“Nimechoka kurudisha fedha kwa wapangaji, mimi nategemea nyumba  hii kupata pesa za kuendeshea maisha yangu.
“Wakati fulani nashindwa kuwarudishia fedha kwani nakuwa nimeshazitumia na hapo ndiyo mgogoro unapoanza, wapangaji wengine huondoka hata bila kunidai wakiamini mimi ndiye nashirikiana na hayo majitu.
Akisimulia muda wa sauti hizo kuanza, mwanamke huyo alisema: “Mara nyingi huanza saa 12 jioni wapangaji wanapoanza kuingia bafuni kuoga. Kwa kweli napata tabu na nyumba yangu.
“Wapangaji wanaogopa, hawalali usiku kwani wakati fulani husikika sauti kama ya bundi huku moto mkali ukionekana ukiwaka bila chanzo chake kujulikana.
“Sasa hivi nimebaki na mpangaji mmoja tu ambaye si kwamba jasiri bali anasubiri nimrudishie fedha zake. Nimechoka na haya majitu, sasa niende wapi au nifanyeje? Siwezi kuikimbia nyumba yangu.
 “Nilishakwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ (Dar) lakini wakasema wao hawawezi kushughulika na kesi ya mauzauza.
“Siku nyingine nikaenda kwa mjumbe wangu, Peter Sabato Sanju wa Shina Namba 7, Tawi la Sinza ‘D’ naye alisema hawezi kushughulika na watu wasioonekana. Nimehangaika hadi makanisani nako sijaona tofauti.
Mjumbe Sanju alipohojiwa na Uwazi alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mama huyo lakini alishindwa kuyashughulikia madudu hayo kwa sababu hayaonekani hivyo alimshauri aende kanisani kwa ajili ya maombi.
“Ni kweli aliwahi kuja kuniambia, lakini tatizo ni kwamba, sauti za ajabu zinasikika lakini huoni watu wala kitu, nikamwambia aende kanisani akaombewe,” alisema mjumbe huyo.

Post a Comment

أحدث أقدم