Niaje…niaje
watu wa Mungu? Tupo vizuri…si ndiyo eeh. Basi sawa kozi kona hii ni
mzuksi kinomanoma. Ama nene? Basi ni mpango mzima wana. Hapa ni mwendo
wa kusanuka na kama vipi ukiona spidi ni kubwa unaruhusiwa kuomba poo.
Usijidai kukomaa utapasuka bure. Huu mziki mnene wazazi.
Tudei bana ngoja tupige mastori moo ya masela wa tauni. Najua samu
pipo tena makachaa wangu kabisa dizaini kama watanimaindi bati kama
mbwai iwe mbwai tu, mkimaindi kimpango wenu makachaa. Sasa mimi si ndo
jembe lenu la kuwasanua?
Ebana kuna ishu moko ambayo naona kama inazingua mashori. Eti msela
ana mbebiz wake kitu na boksi kabisa na wamesavaivu kwa miaka bee bati
anaogopa kumpeleka kwa fasi ya geto.Kuna ishu ambayo masela
hawajashtuka. Unanyaka kwamba shori anapoona kaka mkubwa hataki
kumpeleka kwa mahomu kwake, anakuwa na mawazo diferenti kuhusu kachaa.
Festi, anajua labda msela ana mai waifu kitu cha famili au anachili
na manzi mwingine so hataki shori awe anapajua skani. Ukweli ni kwamba
shori anaweza akawa anahisi vitu kibwena ikiwemo kujiona labda si mkare
au hana hadhi ya kuoneshwa geto.
Enewei, vyote hivyo vinawezekana bati niamini mimi kuwa mageto ya
baadhi ya washkaji hayaingiliki. Chukua hiyo kutoka kwangu. Kama siyo
kwamba mageto hayana hadhi basi ujue mazingira si salama so masti
ujiweke mbali na watoto wazuri.
Anayebisha kwamba baadhi ya mageto ya wana ni machafu anyooshe
kidole! Thubutu yako! Siyo sekreti mazee baadhi ya mageto ya wana ni
aibu ileile.Chukua kutoka kwangu kuwa mageto mengi ya washkaji ni
machafu hatare kiasi kwamba kama akimpeleka shori haliingiliki! Achilia
mbali mazingira machafu na harufu kali, ukizama kwa rumu hicho kitanda
chenyewe kipo vululuvuluu.
Mazee si ajabu ukakuta shuka lina wiki mbili halijafuliwa hadi limechenji rangi jamaa yangu.
Kama manzi akitaka kukorofishana na jamaa yake mwenye laifu la dizaini hiyo, ajifanye kukomaa apelekwe geto uone kama hapajachimbika.
Kama manzi akitaka kukorofishana na jamaa yake mwenye laifu la dizaini hiyo, ajifanye kukomaa apelekwe geto uone kama hapajachimbika.
Mara utasikia pale geto nachili na mshkaji wangu au madogo ilimradi tu asimpeleke mahomu.
Halafu mazee ukikutana na msela kama huyo kitaani ana mbwembwe hatare. Bonge la sharobaro na tisheti ya wasafi klaski mwendo mdudo kumbe geto hakuingiliki au si ajabu mwana kadandia kwa msela wake.
Majembe yangu mmenisoma? Tusimaindiane wana! Kama vipi kitu cha wikiendi hichooo…nduki!

إرسال تعليق