Al Shabab waua afisa wa serikali Mogadishu

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab nchini Somalia wamemuua afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo mjini Mogadishu.

Ripoti zinasema kuwa wanachama wa kundi hilo waliokuwa na silaha wamemmiminia risasi na kumuua Abdifatah Barre aliyekuwa kiongozi wa eneo la Wadajir mjini Mogadishu.

Msemaji wa al Shabab amesema kundi hilo ndilo lililofanya mauaji hayo na amesisitiza kuwa litaendelea kuwaua wapinzani wake mjini Mogadishu.

Vilevile wanachama wa kundi la al Shabab wameshambulia msafara wa Umoja wa Afrika mjini Mogadishu na kusababisha hasara kubwa kwa magari ya msafara huo. Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika walilizingira eneo hilo muda mfupi baada ya shambulizi hilo.

Kundi la kigaidi la al Shabab limezidisha mashambulizi yake mjini Mogadishu katika siku za hivi karibuni.

Post a Comment

أحدث أقدم