Mkuu
wa Wilaya wa Kinondoni, Poul Makonda akiwa na maafisa wa jeshi la
Polisi wakielekea eneo la nyuma jirani na ofisi za madereva..
“Huenda ufahamu…basi tunakufahamisha sasa!!!
Na Andrew Chale,Modewji blog
Matukio kuanzia asunuhi:
Mtandao
wako bora ambao ulipiga kambi ndani ya kituo cha mabasi Ubungo na
kulala hapa hapa, umeweza kukusanyia wewe msomaji wetu matukio muhimu
ambayo yameweza kupatikana kuanzia usiku, asubuhi na hadi mchana
ulipomalizika mgomo huo wa madereva leo Mei 5, majira ya saa sita mchana
mgomo ambao umedumu zaidi ya masaa 31.
Hali
ya usiku ndani ya kituo kulikuwa na baridi kali pia pamoja na mvua mvua
iliyokuwa ikinyesha na kuacha. Abiria wengi walilala kwenye magari
ambayo walikwisha katia tiketi zao huku wengine wakilala kwenye banda la
kusubiria wasafiri wanaowasili na wanaoondoka.
Ndani
ya vibanda vya kiashara hali ilikuwa shwari kabisa kwani kila mmoja
alikuwa akiendelea kupata hiki na kile ikiweo vinywaji na chakula huduma
ambayo ilikuwa ikitolewa muda wote na mud wote watu walikuwa ni wengi.
Vijana wa ‘kihuni’ watulizwa
Hali
ya usalama ilikuwa imeimalishwa hasa kwa vijana wa kihuni pamoja na
watoto wadogo ambao kazi yao kubwa ni kuokotaokota vitu ndani ya kituo
hicho cha mabasi ambapo ulinzi shirikishi walikuwa wakipita kila mahala
ndani ya stendi hiyo katika kuakikisha usalama.
Hata
hivyo baadhi ya magari yaaliweza kuwasha tv, kwa kuweka mikanda na
abiria kuangalia sinema huku wengine wakiwa wamelala. Baadhi ya mabasi
‘classic’ abiria wao hawakupata sana taabu kama wengine kwani wao ndani
ya mabasi yao, waliwasha ‘kipupwe’ na wengine feni huku wakitazama tv
ikiwemo chaneli za kawaida za nje na ndani pia baadhi ya viti vyao
vilikuwa rafiki hata kwa matumizi ya kulala.
Usiku huo ulivyokuwa ukionekana ndani ya kituo hicho cha mabasi Ubungo
Mwanamke kujifungua mtoto
Miongoni
mwa matukio katika mgono huu ni la mwanamke kujifungua mtoto.
Mwanamke huyo, ambaye imeelezwa alikuwa anaelekea katika moja ya mikoa
ya Kusini, alishikwa na uchungu usiku wa manane wakati amelala ndani ya
gari hali iliyopelekea kujifungua huku akisaidiwa na wanawake wengine
waliokuwa pamoja ndani ya gari usiku huo.
‘Hope fail’
Majira
ya saa 10, kasoro usiku huo, baadhi ya abiria walianza kuamshana na
kuamasishana juu ya hatima ya safari zao kama zitakuwapo ama la na wao
wachukue maamuzi. Hata hivyo tumaini lao hilo, lilipotea kadri muda
ulivyozidi kuendelea na kukucha kwani madereva walikuwa wakiwaambia kuwa
kwa sasa gari hazitoondoka mpaka hapo watakapohakikishiwa matakwa yao,
hali ambayo ilizidi kuwanyong’onyesha na kupoteza tumaini kwa habiria
hao ama tunaweza sema ‘hope fail’.
Saa
moja kasoro, baadhi ya mabasai ya Shabiby Line Bus, yaliweza
kuhamasisha abiria wake waingie kwenye magari kwa ajili ya safari, hata
hivyo gari ya kwanza iliyotoka iliweza kusindikizwa kwa ‘eskoti’ huku
ikizomewa katika maeneo ya Ubungo ilipokuwa ikitoka, haata hivyo gari
hilo, kwa mujibu wa watu waliokuwa maeneo ya Mbezi walieleza kuwa,
ilipopolewa mawe, licha ya kuendelea na safari zake ambapo taarifa zaidi
pia tutawaletea kadri zitakapopaatikana kuwa nasi.
Mbali
ya hilo, kuondoka, pia mabasi mengine ya Shabiby, yaliweza kutoka
likiwemo lile lililokuwa likielekea Dodoma pamoja na lile la Msimbati
Line Bus, ambalo ni ndugu na Shabiby Line lililokuwa likielekea Mtwara.
Katika safari hizo za mapema, mabasi hayo ya Shabiby pamoja na yale ya
Dar Express kwa pamoja yaliondoka muda huo wa saa tatu kasoro huku
yakiwa na msafara wa Polisi.
‘Osama akamatwa na Trafiki Ubungo’
Katika
kile ambacho kilionekana kuwa Osama kutaka kufanya yake, Polisi wa
Usalama Barabarani ‘trafiki’ aliweza kumvaa mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la utani Osama na kumkamata baada ya trafiki huyo kumuamulu aondoke
mahalla alipokuwa amesimama jirani na basi la Shabiby.
Osama
alimtolea lugha ya matusi trafiki huyo hali iliyopelekea maafisa
usalama, polisi na mgambo waliokuwa wameweka usalama mahala hapo
kuingilia kati na kumtia nguvuni, lakini Osama ‘aliwadindia’ huku
vijana mbalimbali wapiga debe na abiria wakipiga kelele za kumzomea
askari trafiki kwa kitendo chake cha kutaka kumkamata. Hata hivyo, tukio
hilo lilimalizika kimya kimya baada ya Osama kuachiwa na kisha kuondoka
zake.
Askari
wa Polisi usalama barabarani ambaye jina lake halikupatikana mara moja
akiwa amemkunja ‘Osama’ baada ya wawili hao kutofautiana kiswahili.
‘Waannifahamu’ kizanzibar aaaah.!!
Osama akiwa katika uso wa ‘kummaindi’ trafiki aliyemzingua kituoni hapo.
Abiria wataka kuandamana
Hali
ya abiria baada ya kuona kuwa mbaya, majira ya saa tatu asubuhi,
waliamua kukusanyana makundi huku wakiamasishana waandamane kushinikiza
wasafirishwe. Abiria hao walikuwa na hoja mbalimbali ikiwemo kushinikiza
jeshi hilo kuweza kuwasaidia wasafirishwe ama wachukue hatua baada ya
kuona baadhi ya makampuni ya Shabiby wakianza safari zao huku baadhi ya
magari mengine yakiwa hayajui hatima yake.
Abiria hao wakitoa malalamiko yao kwa mwanahabari juu ya kutaka kufanya maandamano, lakini baadae waliamua kupotezea..
Mwanadada ajitoa ‘muhanga’ kutetea abiria wenzake
Mwanadada
Khadija Muhando, ambaye ni mwenye Albinisimu, aliyekuwa akisafiri
kuelekea Mkoni Arusha, aliweza kupenya na kuingia katikati ya maofisa wa
jeshi la Polisi na kuanza kutoa kilio chake huku akitaka kujua hatima
yao ya safari.
Mwanadada
huyo, alimvaa Kamanda Mkuu wa Usalama barabarani nchini, Kamanda Mpinga
na maofisa wake na kuanza kumlazimisha aamuru madeeva wawasafirishe,
Khadija aliwasumbua mara kwa mara viongozi hao huku wakati mwingine
wakimuama na kwenda kusimama mahala pengine lakini naye aliwaapia kuwa
atakula sahani moja na hadi apate jibu la pamoja.
Khadija
Muhando akionekana kumvaa Kamanda Mpinga ili atoe amri abiria
waruhisiwe kuondoka, licha ya Kamanda Mpinga kumwelezea dada huyo kuwa
mgomo unashughulikiwa asubiri kidogo..
Hali iliendelea kuwa hivi. Kamanda Mpinga na abiria wakizozana juu ya kumaliza mgomo huo..!!
Abiria
Khadija Muhando akiwa anajadiliana na askari kanzu aliyefika eneo hilo,
lakini naye hakufua dafu alimwambia akae pembeni kwani sio saizi yake
katika kile anachokitaka yeye hapo juu ya kupewa jibu sahihi..!
Muafaka bado..!
Hata walivyokuja viongozi, Khadija alikaa pembeni huku akisubiria kuwabana viongozi hao..!
Muafaka bado..!
Mkuu wa Wilaya Poul Makonda awasili Ubungo
Mkuu
wa Wilaya Poul Makonda aliwasili katika kituo hicho majira ya saa nne
asubuhi ambapo baada ya muda waliamua kuwafuaata baadhi ya viongozi wa
madereva na wamiliki waliokuwa wamekaa nyuma kabisa ya kituo hicho cha
mabasi jirani kabisa na ofisi ya madereva.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda alipowaili Ubungo..!
Mkuu wa Wilaya Makonda, akiwasikiliza makamanda wa Polisi wakipanga mikakati..!
Mabomu yapigwa, viongozi wapigwa mawe, chupa
Katika
kile ambacho kinaelezwa mara kwa mara kuwa fujo zinasababishwa na
Polisi dhidi ya raia wema, kimejidhihilisha leo majira ya saa tano
asubuhi Mei 5, baada ya Polisi kuamua kwa makusudi kutumia nguvu ambazo
hazikuwa za lazima katika kuwanyamazisha madereva na wapiga debe
waliokuwa wamejitokeza katika eneo ambalo Maofisa wa Polisi, Mkuu wa
Wilaya Makonda, viongozi wa wamiliki wa mabasi,madereva na wandishi wa
habari, ambapo askaari waliokuwa na mbwa pamoja na mabomu ya machozi
waliweza kufyatua hovyo mabomu hayo na kupiga risasi za moto juu
ilikutawanya watu hao.
Baada
ya mabomu haayo kupigwa, viongozi hao na Makamanda waliamua kulala
chini huku wamekumbatiana , yaani ni tukio ambalo limeingia katika
karne kwani ‘ukomavu’ au ‘ubwanyenye’ wa viongozi wetu ulionekana
katika tukio hili ambalo viongozi hao wote walilala chini sehemu moja
wakiwa wmeshikana huku juu maabomu yakipigwa na mawe yakirushwa kwa
kupigwa wao.
Ni tukio la la dakika 10 hadi 15, watu wane, walijeruhiwa vibaya kwa kupigwa mawe na chupa zilizokuwa zikirushwa na watu hao.
Miongoni
wa watu hao ni madereva ambao mmoja wapo alipasuliwa katika paji la uso
na mwingine kichwani pamoja na kijana mmoja mdogo alijeruhiwa baada ya
mbwa kumng’ata.. HILIKUWA NI PATASHIKA YA AINA YAKE KWANI BAADA YA HAPO
KILA MMOJA ALIOMBA MAJI YA KUNAWA MACHO SI MKUU WA WILAYA AMA KAMANDA
WA POLISI WOTE WALIPATWA NA TAFRANI HIYO.
viongozi hao wakielekea eneo ambalo wangezungumzia muafaka wao huo..!
Mkutano ukiendelea…kabla ya mabomu na kutupiwa mawe hayajaanza..!!
….Mabomu
na kutupiwa mawe yalipoanza. viongozi hao wakakumbuka ‘depo’ na kulala
chini si kamanda wa Polisi Wambura wa Kinondoni wala, Kamanda Mpinga,
ama DC Makonda, wote walilala chini kujinusuru na hali ya usalama.
Tutakuletea video ya tukio!!
Viongozi wakiomba maji ya kunawa usoni…!! hali ilikuwa tete huu ndio umuhimu wa kupitia depo unapohitajika kwa viongozi wengi..!
Hapa waliamua bora watoke eneo hilo kwani si salama.. tena!!
Mbowe wa Chadema awasili na kushangiliwa na umati mkubwa wa madereva
Umati
mkubwa ulikusanyika na kumshangilia Mbunge wa Hai, na Mkuu wa Kambi ya
Upinzani, Freeman Mbowe aliyetinga katika ofisi hizo za madereva na
kuungana na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wialay Makonda na makamanda
wa Polisi wa Kinondoni, usalama barabarani na viongozi wa madereva.
Baada
ya muda kadhaa kupita, wakiwa ndani ya ofisi hizo, wote kwa paamoja
walifikiana hatua ya kukubaliana na kisha wakatoka nje majira ya saa
sita kasoro ambapo walielekea katika eneo maalum na viongozi wa madereva
walitoa maneno kadhaa akiwemo Rashid Salehe na baadae BONGE, ambaapo
baada ya haapo DC Makonda aliamua kuchukua ‘kesi’ hiyo huku akiwaambia
kuwa yeye ni bingwa wa migomo hivyo suala hilo kufika kwake ni sawa na
kwenda kwa mwenye nalo hivyo wampe siku 7 tu, watamaliza matatizo yote
huku akiwataka waache mgomo huo na waendelee na majukumu yao ambapo
endapo pia mambo ya msingi ikiwemo suala la wajumbe wa kamati ya
kushughulikia madai yao hakutakuwa na mtu muhimu wa madereva na
wanayemuamini wao, basi amewaomba warejee katika mgomo huo tena yaani
siku ya Mei 6, saa nne asubuhu.
Mbowe ashangiliwa kila kona!! Washangilia: Rais Rais Rais
Mbowe
akiwa anatoka baada ya kuisha kwa mgomo wa madereva..! huku watu
mbalimbali wakimshangilia na kuimba Rais Rais Rais vijana na pamoja na
abiria waliokuwa ndani ya mabasi.!!
Mbowe akiingia kwenye gari lake ..!
Wakilisukuma
gari lake hilo hadi jirani na hotel ya Blue Peal Ubungo.. na baadae
msafara wa Chadema uliofika Ubungo ulipoondoka ..!
Abiria wakiwa na nyuso zilizokosa matumaini huku wasijue ni muda gani wataondoka, hii ilikuwa majira ya saa tatu asubuhi..!
Mmoja wa madereva akiwa ameshikiliwa baada ya kutokea purukushani na mabomu kupigwa hovyo..!
Mwandishi Mwandamizi wa mtandao huu, Andrew Chale
‘aki-Selfie’ katika aneo la tukio.. ambapo aliweka kambi ndani ya
kituo hicho cha Ubungo na kukusanyia matukio haya ya mgomo huu uliodumu
zaidi ya masaa 31, ambao ni mkubwa na haujawahi kutokea baadala ya ule
wa Aprili 10 mwaka huu ambao wenyewe ulidumu kwa masaa 9 tu. SASA
TUSUBIRI siku saba zilizoahidiwa na Mkuu wa Wilaya Poul Makonda kama
alivyoahidi na utekelezaji wa kushughulikia mgogoro huo. Asante na
Asante wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao huu mara kwa mara, Pia
pongezi ziende kampuni ya tecno kupitia kifaa chao: Pad aina ya P9, tecno ndio iliyowezesha kukupigia picha hizi nzuri na za kukuvutia.
إرسال تعليق