KIJANA mmoja mtanashati, aliyefahamika kwa jina la
Faraja Adam mkazi wa Makongo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni
alinusurika kipigo kutoka kwa wakazi wa Mabibo Jeshini baada ya kukutwa
sebuleni kwa mpangaji wa nyumba moja aliyefahamika kwa jina la Rhobi
Chacha.
Faraja Adam akiomba msamaha baada ya kunaswa.
Majirani wa mpangaji huyo waliliambia gazeti hili kwamba walimuona
kijana huyo akiambaaambaaa na ukuta wa nyumba hiyo kisha kuingia ndani
kwa kunyata, kitu kilichowapa shaka na kuamua kumpigia simu jirani yao
kumweleza juu ya ujio wa kijana huyo.
...wakifungwa kamba pamoja na Jesca ambaye ni mfanya kazi wa ndani kwenye nyumba ya Rhobi.
Majibu waliyopewa na mpangaji huyo yaliwafanya majirani hao
kujikusanya, wakiwemo walinzi wa kimasai wanaolinda maeneo hayo na
alipofika Rhobi, ndipo walipoingia ndani na kupigwa na butwaa kumkuta
‘sharo’ huyo akiwa amejilaza kwenye kochi sebuleni, akiwa ameshikilia
rimoti akiibonyezabonyeza kama yupo nyumbani kwao.
Alipoulizwa kilichompeleka hapo, alikosa cha kujibu, akionekana kuchanganyikiwa.
Alipoulizwa kilichompeleka hapo, alikosa cha kujibu, akionekana kuchanganyikiwa.
...kamba ikikazwa ili kupelekwa kituo cha polisi.
Baada ya kutishiwa kipigo cha kumwitia mwizi kwa kuingia kwa watu
bila wenyewe kuwepo, aliomba aachwe kwa maelezo kuwa alimfuata dada wa
kazi wa nyumba hiyo.
...wakipelekwa Kituo cha Polisi cha Urafiki.
“Jamani mimi nina ndugu zangu wakubwa sana serikalini, naomba
msinifanye chochote kile, nimekuja kwa Jesca (house girl) kwani ni
dadangu kabisa,” alijitetea kijana huyo.
...wakipelekwa kwenye Kituo cha Polisi.
Jesca baada ya kuulizwa uhusiano wake na kijana huyo alikosa cha
kusema, lakini simu yake ya mkononi ilipopekuliwa, ilikutwa ikiwa na
meseji alizokuwa akitumiana na kijana huyo, zilizoashiria mapenzi.
Baadaye wawili hao walidhibitiwa na kupelekwa kituo cha Polisi cha
Urafiki ambako mzazi wa Faraja alipoitwa, alitaka mwanaye huyo alazwe
rumande ili iwe fundisho kwake aachane na tabia hiyo.
Naye Rhobi, aliliambia gazeti hili kuwa tabia ya msichana wake huyo
wa kazi imebadilika katika siku za hivi karibuni na kwamba mara kadhaa,
amekuwa akikuta kitanda chake kikiwa kimevurugika tofauti na
alivyokiacha.
إرسال تعليق