Kiongozi
wa madereva nchini, Rashid Said, akiongea na umati wa madereva kaatika
sakata hilo ambapo alikuwa akitoa ufafanuzi na namna ya kumsubiria
Waziri Mkuu Mizengo Pinda afike eneo hilo kuongea na madereva hao.
News Alert; MUDA
HUU SAA KUMI NA DAKIKA 19 !!!!!!MABOMU MABOMU MABOMU !!! ASKARI POLISI
SASA HIVI WANAPIGA MABOMU YA MACHOZI OVYO, TAYARI WAMEPIGA MAWILI WATU
WANAKIMBIA OVYO!
ABIRIA WALIOKUWA WANAENDA OFISI ZA SUMATRA WAMEPIGWA MABOMU YA MACHOZI WAKIWATAWANYA.
**Mgomo kuwa wa muda mrefu zaidi: madereva wasema hata wakikaa siku tatu watakula biskuti
Na Andrew Chale, Modewji blog
Kutoka
eneo la Ubungo na maeneo ya jirani na Dar es Salaam ni kuwa mgomo hadi
muda huu tayari umekuwa mkubwa baada ya ule wa mwezi uliopita kudumu
zaidi ya masaa 9, lakini huu wa leo tayari umefikisha masaa 9, lakini
kukiwa hakuna dalili zozote za kufikia muafaka hadi sasa baada ya
mashinikizo ya madereva hao kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufika
katika kituo hicho kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani cha
Ubungo, jijini Dar es Salaam, ilikutoa tamko la madai yao.
Modewji
ambayo ipo hapa imepiga kambi tokea mapema asubuhi ya leo, imeendelea
kushuhudia madereva hao wakiwa wamejikusanya makundi kwa makundi na
wengine kushika mabango mbalimbali wakiwa na hamu na shahuku ya
kumsubiria Waziri Mkuu Pinda.
Kwa
mujibu wa madereva hao, kupitia kwa kiongozi wao, Rashid Said
aliwatangazia madereva hao kuwa mgomo huo utaendelea hadi hapo Waziri
Mkuu Pinda atakapofika kuongea nao.
“Tutakaa
hapa hapa. Hadi hapo Waziri Mkuu Pinda atakapokuja kuongea na sisi.
Kama hatofika basi mgomo huu utakuwa endelevu hadi muafaka ufike!!”
alieleza Rashid Saidi huku akishangiliwa kwa nguvu kubwa na madereva
hao.
Kwa
sasa eneo la Ubungo miuondombinu ni mibovu huku maji machafu ya mvua
yakizagaa hovyo, ambapo baadhi yao wameendelea kulalamikia Serikali kuwa
inakusanya kodi zao za bure ikiwemo ushuru huku kituo kikiwa kichafu
ambapo pia wamebainisha kuwa, wameambiwa waziri Mkuu hawezi kufika
kwenye kituo hicho kutokana na kuwa ni pachafu.
Kauli
hiyo ya kudaiwa mahala hapo ni pachafu ndio maana Waziri Mkuu
anashindwa kufika, imechukuliwa kwa hisia tofauti na madereva hao huku
kila mmoja akishindwa kuamini kama imetolewa na Pinda ama ni msaidizi wa
Pinda.
Kwa
upande wake mmoja wa viongozi wa madereva hao, maarufu kama BONGE,
ambaye amekuwa akikubalika sana na madereva hao alipanda juu ya jukwaa
na kisha kuwatangazia madereva wenzake kuwa, Mgomo huo utaendelea bila
kikomo hata ukiwa wa siku tatu, watakula biskuti na siku itaenda.
“MADEREVA!
TUPO PAMOJA. TUTAKAA HAPA HADI PINDA AFIKE. NA ASIPOFIKA TUNAO UWEZO WA
KUKAA HAPA BILA KUFANYA KAZI NA TUKASHINDIA BISKUTI!! SI TUNAWEZA!!!”
aliuliza na kuitikiwa kwa shangwe na madereva wenzake. NDIOO NDIO HAPA
HATOKI KIONGOZI YOYOTE WA KWENDA KWA WAZIRI PINDA, TUTAKAA HAPA HAPA
HADI KIELEWEKE! WALISEMA MADEREVA HAO.
Hata
hivyo, licha ya mgomo wa Mwezi Aprili mwaka huu kuwa na msululu wa
magari ya Polisi na viongozi wao pamoja na viongozi wa Serikali, lakini
kwa siku ya leo hakuna kiongozi hata mmoja wa Kitaifa ama wa Serikali
aliyefika kuongea na madereva hao.
Ila
kwa hali ya nje, ni umati mkubwa wa watu wakiwemo wasafiri na wapita
njia wakiendelea kusubiria hali ya mgomo, gari za Polisi zimetaanda kila
mahala, ambapo majira ya saa 5 asubuhi, Polisi walipiga bomu moja la
machozi katika eneo la Ubungo maji ambapo kulikuwa na hali ya
kutoelewana ya tafrani na kuisha.
Taarifa zaidi zitakuwa zinaendelea kadri ya inapotokea kutoka hapa.
Mmoja
wa viogozi wa madereva maarufu’ BONGE’ akiwatuliza madereva hao. BONGE
amekuwa na msimamo ambapo karibu madereva wengi wamekuwa wakimkubali kwa
msimamo wake huo.
Mwandishi Mwandamizi wa Modewji blog Andrew Chale, akiwa katika heka heka za kuchukua picha za mgomo huo wa madereva kwa nyuma na chini ni baadhi ya mabango ya madereva hao
Madereva hao wakiwa na mabango yao!!
!!!!!!MABOMU
MABOMU MABOMU !!! ASKARI POLISI SASA HIVI WANAPIGA MABOMU HOVYO YA
MACHOZI TAYARI WAMEPIGA MAWILI WATU WANAKIMBIA HOVYO
Post a Comment