Mgomo wa madereva: Mabomu ya Machozi Jana Yalilindima Ubungo- Mambo yalikuwa Hivi

IMG_20150504_131123
Kiongozi wa madereva nchini, Rashid Said, akiongea na umati wa madereva kaatika sakata hilo ambapo alikuwa akitoa ufafanuzi na namna ya kumsubiria Waziri Mkuu Mizengo Pinda afike eneo hilo kuongea na madereva hao.
News Alert; MUDA HUU SAA KUMI NA DAKIKA 19 !!!!!!MABOMU MABOMU MABOMU !!! ASKARI POLISI SASA HIVI WANAPIGA MABOMU YA MACHOZI OVYO, TAYARI WAMEPIGA MAWILI WATU WANAKIMBIA OVYO!
ABIRIA WALIOKUWA WANAENDA OFISI ZA SUMATRA WAMEPIGWA MABOMU YA MACHOZI WAKIWATAWANYA.

 **Mgomo kuwa wa muda mrefu zaidi: madereva wasema hata wakikaa siku tatu watakula biskuti

 Na Andrew Chale, Modewji blog
Kutoka eneo la Ubungo na maeneo ya jirani na Dar es Salaam ni kuwa mgomo hadi muda huu tayari umekuwa mkubwa  baada ya ule wa mwezi uliopita kudumu zaidi ya masaa 9, lakini huu wa leo  tayari umefikisha masaa 9, lakini kukiwa hakuna dalili zozote za kufikia muafaka hadi sasa baada ya mashinikizo ya madereva hao kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufika katika kituo hicho kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, ilikutoa tamko la madai yao.
Modewji ambayo ipo hapa imepiga kambi tokea mapema asubuhi ya leo,  imeendelea kushuhudia madereva hao wakiwa wamejikusanya makundi kwa makundi na wengine kushika mabango mbalimbali wakiwa na hamu na shahuku ya kumsubiria Waziri Mkuu Pinda. 
Kwa mujibu wa madereva hao, kupitia kwa kiongozi wao, Rashid Said aliwatangazia madereva hao kuwa mgomo huo utaendelea hadi hapo Waziri Mkuu Pinda atakapofika kuongea nao.
“Tutakaa hapa hapa. Hadi hapo Waziri Mkuu Pinda atakapokuja kuongea na sisi. Kama hatofika basi mgomo huu utakuwa endelevu hadi muafaka ufike!!” alieleza Rashid Saidi huku akishangiliwa kwa nguvu kubwa na madereva hao.
Kwa sasa eneo la Ubungo miuondombinu ni mibovu huku maji machafu ya mvua yakizagaa hovyo, ambapo baadhi yao wameendelea kulalamikia Serikali kuwa inakusanya kodi zao za bure ikiwemo ushuru huku kituo kikiwa kichafu ambapo pia wamebainisha kuwa, wameambiwa waziri Mkuu hawezi kufika kwenye kituo hicho kutokana na kuwa ni pachafu.
Kauli hiyo ya kudaiwa mahala hapo ni pachafu ndio maana Waziri Mkuu anashindwa kufika, imechukuliwa kwa hisia tofauti na madereva hao huku kila mmoja akishindwa kuamini kama imetolewa na Pinda ama ni msaidizi wa Pinda.
Kwa upande wake mmoja wa viongozi wa madereva hao, maarufu kama BONGE, ambaye amekuwa akikubalika sana na madereva hao alipanda juu ya jukwaa na kisha kuwatangazia madereva wenzake kuwa, Mgomo huo utaendelea bila kikomo hata ukiwa wa siku tatu, watakula biskuti na siku itaenda.
“MADEREVA! TUPO PAMOJA. TUTAKAA HAPA HADI PINDA AFIKE. NA ASIPOFIKA TUNAO UWEZO WA KUKAA HAPA BILA KUFANYA KAZI NA TUKASHINDIA BISKUTI!! SI TUNAWEZA!!!” aliuliza na kuitikiwa kwa shangwe na madereva wenzake. NDIOO NDIO  HAPA HATOKI KIONGOZI YOYOTE WA KWENDA KWA WAZIRI PINDA, TUTAKAA HAPA HAPA HADI KIELEWEKE! WALISEMA MADEREVA HAO.
Hata hivyo, licha ya mgomo wa Mwezi Aprili  mwaka huu kuwa na  msululu wa magari ya Polisi na viongozi wao  pamoja na viongozi wa Serikali, lakini kwa siku ya leo hakuna kiongozi hata mmoja wa Kitaifa ama wa Serikali aliyefika kuongea na madereva hao.
Ila kwa hali ya nje, ni umati mkubwa wa watu wakiwemo wasafiri na wapita njia wakiendelea kusubiria hali ya mgomo, gari za Polisi zimetaanda kila mahala, ambapo majira ya saa  5 asubuhi, Polisi walipiga bomu moja la machozi katika eneo la Ubungo maji ambapo kulikuwa na hali ya kutoelewana ya tafrani na kuisha.
Taarifa zaidi zitakuwa zinaendelea kadri ya inapotokea kutoka hapa.
ee
Mmoja wa viogozi wa madereva maarufu’ BONGE’ akiwatuliza madereva hao. BONGE amekuwa na msimamo ambapo karibu madereva wengi wamekuwa wakimkubali kwa msimamo wake huo.
an
Mwandishi Mwandamizi wa Modewji blog Andrew Chale, akiwa katika heka heka za kuchukua picha za mgomo huo wa madereva kwa nyuma  na chini ni baadhi ya mabango ya madereva hao
aa
weee
Madereva hao wakiwa na mabango yao!!
!!!!!!MABOMU MABOMU MABOMU !!! ASKARI POLISI SASA HIVI WANAPIGA MABOMU HOVYO YA MACHOZI  TAYARI WAMEPIGA MAWILI WATU WANAKIMBIA HOVYO

Post a Comment

أحدث أقدم