Waziri
wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kulia), akikata
utepe kuzindua rasmi Taasisi ya maendeleo ya jamii ya Sitti Tanzania
Foundation iliyofanyika Dar es Salaam juzi (kushoto) ni Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo, Sitti Mtemvu.
Na Mwandishi Wetu, Mpekuzi-Dar es Salaam
WAZIRI
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema kuwa
kutokana na hali ya nchi kwa sasa Rais Jakaya Kikwete, atasaini sheria
ya mtandao.
Kauli
hiyo aliitoa jana baada ya kuripotiwa na gazeti moja la kila siku
mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Kitabu cha Chozi la Sitti, ambapo
alinukuliwa akisema kuwa Rais Kikwete ameshasaini sheria hiyo.
Akikanusha
taarifa hiyo alisema kuna uwezekano amenukuliwa vibaya ila usahihi wa
kile alichosema ni kwamba Rais ataisaini sheria hiyo kutokana na hali ya
usalama wa nchi kwa sasa.
“Nilishosema si kwamba sheria imesainiwa,
maana kwa mujibu wa utaratibu wa sheria ni kwamba sheria yoyote rais
akishaisaini inapelekwa taarifa kwa Spika wa Bunge ambaye naye
huitangaza.
“Kwa
hiyo nami katika uzinduzi ule nilisema kama kukazia kauli ya Ikulu kuwa
Rais Kikwete ataisani sheria ile kwani imefuata taratibu zote, ikiwemo
kujadiliwa bungeni na hatimaye kuridhiwa.
“Hivyo ninawaomba Watanzania, waelewe kuwa hiki ndicho nilichokisema na si vinginevyo,” alisema Sophia.
Waziri
huyo alisema pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kuleta maendeleo na
kusambaza taarifa kwa muda mfupi, lakini kuna watu wamekuwa wakiitumia
vibaya ikiwemo kuchafuana huku anayeathirika akishindwa kuchukua hatua
za kisheria.
Pamoja
hatua hiyo wadau wengi wamekuwa wakimshauri Rais Jakaya Kikwete
asiisaini sheria ili kwani inaminya na hata kunyonga uhuru wa habari
nchini.
إرسال تعليق