SOMA HAYA YA Emmanuel Adebayor na familia yake UJIFUNZE KITU KATIKA MAISHA

Emanuel na mamake mzazi
Miezi michache tu baada ya kumlaumu mamake mzazi kwa kumroga na kumfanya apoteze fomu yake, Emmanuel Adebayor anayeichezea timu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, amejitokeza na kufichua jinsi familia yake ilivyomfanya afilisike bila shukrani.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Adebayor ameeleza kuwa
"Nimekuwa nikiziweka taarifa hizi kwa muda mrefu lakini leo nimehisi kuwa ni muhimu kuwaeleza nanyi pia. Ni ukweli kuwa masuala ya familia hayastahili kuwekwa hadharani lakini nafanya hivi ili familia nyingine nzao zipate funzoi kupita yaliyonisibi. Aliandika
Anasema wakati alipokuwa na umri wa miaka 17, aliutumia mshahara wake wa kwanza kuijengea familia yake nyumba.Kama mnavyojua nilipokea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka mwaka 2008.Nilimpandisha mama yangu jukwaani kumshukuru yeye kwa mambo yote. Mwaka ule ule nilimleta London kwa ajili uchunguzi wa afya yake.
Wakati binti yangu alipozaliwa niliwasiliana na mama yangu kumweleza lakini alikata simu na sikujua ni kwanini.Soma maoni yangu ya hivi karibuni watu wanasema mimi na familia yangu twende tupate ushauri kwa mhubiri maarufu wa dini ya kikristo T.B Joshua.Mwaka 2013 nilimpa mama yangu pesa ili aende kupata ushauri kwa mhubiri huyo nchini Nigeria.
Alipaswa kukaa huko kwa wiki moja, lakini siku mbili tu alipofika nilipokea simu kwamba ameondoka. Zaidi ya hayo nilimpa mama yangu pesa nyingi kuanzisha biashara kupika pamoja na bidhaa nyingine. Kiuhalisia niliwaruhusu kuweka jina langu na picha yangu kwenye biashara hiyo hiyo ili waweze kuvutia wateja.
Ni kitu gani kingine mtoto wa kiume anaweza kufanya ndani ya uwezo wake kusaidia familia yake?
Miaka kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba huko East Lagon nchini Ghana kwa dola milioni 1.2 za kimarekani. Nikaona ni sawa dada yangu mkubwa Yabo Adebayor kuishi katika nyumba hiyo. Vile vile nilimruhusu kaka yangu Daniel naye aishi kwenye nyumba hiyo.
Emanuel Adeboyor akiwa na mama yake mzazi
Miezi michache baadae nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa naishi ikianibidi kwenye hiyo nyumba yangu. Kilichonishangaza niliona magari mengi kwenye barabara. Kwa kweli dada yangu aliamua kuikodisha hiyo nyumba pasipo kunieleza. Alimfukuza Daniel kwenye hiyo nyumba.
Mfahamu kwamba nyumba hiyo ina vyumba 15. Nilipompigia dada yangu anipe ufafanuzi alichukua karibu nusu saa kunishambulia na kunitukana kwenye simu. Nilimpigia mama yangu anaelezee kisa kizima naye akafanya kama dada yangu alivyofanya. Hivyo ni kama dada yangu alivyosema sina shukrani.
Kaka yangu Kola Adebayor, anaishi nchini Ujerumani kwa miaka ishirini na mitano sasa,safari zake zote za kurejea nyumbani mara nne ametumia gharama zangu,kama hiyo haitoshi ninawasomesha watoto wake na kuwalipia gharama zote kuhusiana na elimu yao.
Nilipokuwa nchini Monaco ,alinifuata na kutaka pesa za kuanzishia biashra yake .Mungu pekee ndiye ajuaye nilimpa kiasi gani cha kufungulia biashara yake,kama ukimuuliza biashara hiyo iko wapi leo?
Masahibu hayakuishia hapo,kaka yetu Peter alipoaga dunia nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha pesa ili arejee nyumbani,cha kushangaza hakutokea msibani ama siku ya maziko.na leo kaka yule yule (Kola) anawaambia watu kuwa chanzo cha kifo cha kaka yetu Peter ni mimi,linawezekanaje hili? Kaka huyu huyu alikwenda kwenye gazeti la"The Sun" na kueleza habari za uongo kuhusiana na familia yetu ili kujipatia fedha.
Wakatuma barua pia katika klabu ya mpira ya Madrid nikafukuzwa.nilipokuwa nchini humo pia nilipata wazo kuwa ni vyema kuwa na familia ya wana soka,hivyo nikahakikisha kaka yangu Rotimi anajiunga na chuo cha mafunzo ya mpira huko Ufaransa. Miezi michache tu,wachezaji ishirini na saba wa chuo hiyo aliwaibia simu za mkononi wachezaji ishirini na mmoja .Sikuongea chochote kuhusiana na kaka Peter Adebayor ,kwasababu hayuko nasi leo hii,Mungu ailaze mahala pema peponi ,amina.
Dada yangu sasa, Lucia Adebayor amekuwa na tabia ya kuwaambia watu kuwa baba yetu amenitaka nimchukue dada huyu na kumpeleka ulaya,lakini sababu kubwa hasa ni nini ya kumpeleka huko ulaya? Kila aliyeko hapa yupo kwa sababu.
Nilirejea nyumbani Ghana nilipata taarifa za kaka yangu anaumwa sana,niliendesha gari kwa kasi sana kuelekea Togo ili kukutana naye na kumpa msaada anaostahili,nilipowasili huko mama yangu akanikatalia kumwona na kunieleza kuwa ninachopaswa kufanya ni kumpa mama yangu pesa nay eye ata maliza kila kitu.
Mungu pekee ndiye ajuaye siku ile ile nikampatia mama yangu kiasi cha pesa alichokitaka,lakini cha ajabu watu wanalalama kuwa sikufanya lolote kuokoa maisha ya kaka yangu Peter.je mimi ni mpumbavu kiasi gani niendeshe gari mpaka Togo bure bila ya sababu?
Nikaandaa mkutano wa kifamilia mwaka 2005 ili tumalize tofauti zetu na matatizo yanayotuzunguuka.nilipowauliza maoni yao wakanitaka kuwajengea nyumba kila mmoja wao na mishahara mikubwa kila mwezi kwa kila mmoja wao.
Leo hii niko hai wamejimilikisha kila kilicho change je nikifa itakuwaje?kwa sababu zote hizi,itanichukua muda mrefu mno kuweka mikakati na misingi yangu barani Africa.kila wakati ninajitahidi kuwasaidia wahitaji,familia yangu wao huhoji kila nifanyacho na wote huona nimefanya uamuzi mbaya.
Ikiwa leo ninaandika haya,sina lengo la kuwaanika watu wa familia yangu.ninataka familia zingine za kiafrika kujifunza kutokana na ninayoyapitia mimi. Asanteni sana.

Post a Comment

أحدث أقدم