XXL ni show ambayo inaruka #OnAiR kila
siku kuanzia saa 7 mchana mpaka 10, Jumatatu mpaka Ijumaa.. 255 ni
sehemu ya show hiyo ambayo inakuwa na story mbalimbali za burudani..
labda umepitwa na ya leo !!
Ilikuwa na majina ya mastaa hawa wa TZ, One the Incredible, Linex na Wema Sepetu.
Tumesikia kwamba album za Bongofleva zinarudi sokoni, rapper One amesema hicko ni kitu kizuri sana ambapo kwa msanii kuwa na idadi ya album kadhaa sokoni ni kama CV yake hivi.
Linex
mkali mwingine wa muziki amesema aliandikiwa barua kutoka Hospitali ya
Kabanga iliyoko Kigoma, wakamuomba awe Balozi wao.. Hospitali hiyo
inategemewa na watu wengi wa Kigoma, jamaa aliamua kuitembelea Hospitali
hiyo na kutroa msaada kutokana na hali abayo aliiuta kwenye Hospitali.
Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu
aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu ishu ya Sheria ya
Matumizi ya Mitandao kwamba hayuko tayari kuona fans wake
wananyang’anywa haki zao.
Wema
kasema alitoa maoni hayo sio kwa sababu anawatetea watu ambao
wanaandika vitu vibaya mitandaoni, hata yeye ni mmoja ya wanaoandikwa
vibaya na watu hao ambao wengine wanajiita #TeamWEMA lakini yeye
hawajui.. Wema amesema anachokikubali kwa watu hao ni mapenzi yao kwake na sio kitu kingine.
255 iko pia kwenye sauti hii ambayo hata wewe unaweza kuiplay kuisikiliza
إرسال تعليق