Airtel Rising Star Awamu Ya Pili Yazinduliwa

Kampuni ya simu za mkononi ya airtel Tanzania pamoja na timu ya soka ya Manchester United ya nchini Uingereza leo asubuhi wamezindua awamu ya pili ya mradi wa kuendeleza mpira wa miguu barani Africa unaoitwa Airtel Raising Star phase two katika hoteli ya kimataifa ya Sea cliff.
Mradi huo ambao unahusisha vijana walio chini ya umri wa miaka 17 katika nchi 16 ambazo mtandao huo unapatikana umezinduliwa baada ya ule wa mara ya kwanza ambao ulifanyika mwaka jana kwa mafanikio na hivyo kuwashawishi wadhamini hao Kampuni ya Airtel pamoja na
timu ya Manchester United kuendelea na awamu ya pili.
Akizungumza katika sherehe ya kuzindua awamu hiyo ya pili Mkurugenzi wa Kampuni ya Airtel Tanzania bwana Sam Elangallor alisema kutokana na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana ambapo karibu timu 11,000 zilishiriki katika mchujo wa kuingia kwenye mashindano kutoka pembe zote, hiyo ni ishara tosha kuwa mashindano hayo yanaunganisha jumuiya mbali mbali pamoja na kutoa fursa ya kupata mafunzo na kutimiza ndoto za kimichezo kwa wale wanaokidhi vigezo.
Akiendelea bwana Sam alisema kwa mwaka huu wataendelea na program ile ile kama ya mwaka jana ambapo mashindano yataandaliwa katika mfumo wa mechi za timu za nchi kwa nchi na pia timu zilizo ndani ya nchi husika kabla ya kambi ya mafunzo ambayo kwa mwaka huu itafanyika jijini Nairobi nchini Kenya chini ya ukufunzi wa makocha kutoka timu ya Manchester United ambapo timu za vijana wa kike na kiume zitachuana kwa siku nne.
Aidha Mkurugenzi wa kamati ya Mashindano kutoka chama cha soka Tanzania (TFF) , bwana Kawemba Saadi alisema wao wamefurahishwa na uzindizi wa mradi huo kwani ni sehemu ya uendelezaji wa program ambazo zinasaidia kutoa vipaji kwenye timu ya taifa na hivyo anawapongeza Airtel Tanzania kwa kuwa wadhamini wakuu na wao Tff ambao ni walezi wa mpira nchini watasimamia mchakato huo kwa Tanzania kwa kupitia Chama cha soka mkoa wa ilala yaani DRFA.
Naye Mgeni Rasmi wa sherehe hiyo ya uzinduzi wa awamu hiyo ya pili ya mradi wa Airtel Rising Star, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia prof Makame M Mbarawa alisema yeye kama waziri wa Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefarijika sana na mradi huo kwani unaongeza wigo wa ajira pamoja na kuchangia katika sera ya maendelo ya michezo nchini. Aliwashukuru Pia timu ya Manchester united kwa kushirikiana na Airtel katika kufanikisha mradi huo maalum kwa ajili ya vijana .
Akichangia katika risala walizotoa waliomtangulia mchezaji nguli aliyewahi kuchezea Manchester united miaka ya nyuma Bwana Quinton Fortune alisema yeye amefurahia kuwa mmoja ama sehemu ya mradi huo ambapo yeye anachukuliwa kama kioo kwani yeye ni mmoja wa wachezaji waliopitia mfumo wa namna hiyo na ndio maana ameteuliwa kuwa mmoja wa wahamasishaji ili kuwaonyesha njia wale wanaotaka kupatanafasi ya kucheza kwenye timu kubwa kama Manchester United.
Akimalizia katika kutoa hotuba kutoka meza kuu mwakilishi wa Timu ya Manchester United ambaye ni Mkurugenzi wa Biashara bwana Richard Arnold alisema amefurahiswa na ushirikiano huo kati ya timu ya Manchester United Na airtel na kwamba wao kama timu wataendelea kutoa sapoti kwa airtle ambapo anasema mradi huo ulipata mafaniko makubwa sana baada ya kushuhudia vipaji vya hali ya juu kutoka nchi mbali mbali za Africa ambapo mradi huo unafanyika.
Usajili kwa ajili ya mradi huu wa airtel Rising Star awamu ya pili unaanza Tarehe 14 mwezi huu ambapotimu 24 zinatarajiwa kupambana kutoka Kanda 6 za kimashindano ambazo ni pamoja na Lindi, Mbeya, Arusha, Kinondoni, Ilala na Temeke.

Post a Comment

Previous Post Next Post