
Kampuni ya simu za mkononi ya airtel Tanzania pamoja na timu ya soka
ya Manchester United ya nchini Uingereza leo asubuhi wamezindua awamu ya
pili ya mradi wa kuendeleza mpira wa miguu barani Africa unaoitwa
Airtel Raising Star phase two katika hoteli ya kimataifa ya Sea cliff.
Mradi huo ambao unahusisha vijana walio chini ya umri wa miaka 17
katika nchi 16 ambazo mtandao huo unapatikana umezinduliwa baada ya ule
wa mara ya kwanza ambao ulifanyika mwaka jana kwa mafanikio na hivyo
kuwashawishi wadhamini hao Kampuni ya Airtel pamoja na
timu ya
Manchester United kuendelea na awamu ya pili.
Akizungumza katika sherehe ya kuzindua awamu hiyo ya pili Mkurugenzi
wa Kampuni ya Airtel Tanzania bwana Sam Elangallor alisema kutokana na
mafanikio yaliyopatikana mwaka jana ambapo karibu timu 11,000
zilishiriki katika mchujo wa kuingia kwenye mashindano kutoka pembe
zote, hiyo ni ishara tosha kuwa mashindano hayo yanaunganisha jumuiya
mbali mbali pamoja na kutoa fursa ya kupata mafunzo na kutimiza ndoto za
kimichezo kwa wale wanaokidhi vigezo.
Akiendelea bwana Sam alisema kwa mwaka huu wataendelea na program ile
ile kama ya mwaka jana ambapo mashindano yataandaliwa katika mfumo wa
mechi za timu za nchi kwa nchi na pia timu zilizo ndani ya nchi husika
kabla ya kambi ya mafunzo ambayo kwa mwaka huu itafanyika jijini Nairobi
nchini Kenya chini ya ukufunzi wa makocha kutoka timu ya Manchester
United ambapo timu za vijana wa kike na kiume zitachuana kwa siku nne.
Aidha Mkurugenzi wa kamati ya Mashindano kutoka chama cha soka
Tanzania (TFF) , bwana Kawemba Saadi alisema wao wamefurahishwa na
uzindizi wa mradi huo kwani ni sehemu ya uendelezaji wa program ambazo
zinasaidia kutoa vipaji kwenye timu ya taifa na hivyo anawapongeza
Airtel Tanzania kwa kuwa wadhamini wakuu na wao Tff ambao ni walezi wa
mpira nchini watasimamia mchakato huo kwa Tanzania kwa kupitia Chama cha
soka mkoa wa ilala yaani DRFA.
Naye Mgeni Rasmi wa sherehe hiyo ya uzinduzi wa awamu hiyo ya pili ya
mradi wa Airtel Rising Star, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na
Teknolojia prof Makame M Mbarawa alisema yeye kama waziri wa Serikali ya
jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefarijika sana na mradi huo kwani
unaongeza wigo wa ajira pamoja na kuchangia katika sera ya maendelo ya
michezo nchini. Aliwashukuru Pia timu ya Manchester united kwa
kushirikiana na Airtel katika kufanikisha mradi huo maalum kwa ajili ya
vijana .
Akichangia katika risala walizotoa waliomtangulia mchezaji nguli
aliyewahi kuchezea Manchester united miaka ya nyuma Bwana Quinton
Fortune alisema yeye amefurahia kuwa mmoja ama sehemu ya mradi huo
ambapo yeye anachukuliwa kama kioo kwani yeye ni mmoja wa wachezaji
waliopitia mfumo wa namna hiyo na ndio maana ameteuliwa kuwa mmoja wa
wahamasishaji ili kuwaonyesha njia wale wanaotaka kupatanafasi ya
kucheza kwenye timu kubwa kama Manchester United.
Akimalizia katika kutoa hotuba kutoka meza kuu mwakilishi wa Timu ya
Manchester United ambaye ni Mkurugenzi wa Biashara bwana Richard Arnold
alisema amefurahiswa na ushirikiano huo kati ya timu ya Manchester
United Na airtel na kwamba wao kama timu wataendelea kutoa sapoti kwa
airtle ambapo anasema mradi huo ulipata mafaniko makubwa sana baada ya
kushuhudia vipaji vya hali ya juu kutoka nchi mbali mbali za Africa
ambapo mradi huo unafanyika.
Usajili kwa ajili ya mradi huu wa airtel Rising Star awamu ya pili
unaanza Tarehe 14 mwezi huu ambapotimu 24 zinatarajiwa kupambana kutoka
Kanda 6 za kimashindano ambazo ni pamoja na Lindi, Mbeya, Arusha,
Kinondoni, Ilala na Temeke.
- Airtel Managing Director akizichapa na Quinton Fortune
- Airtel Tz Managing Director
- Quintone Fortune Greating a fan


إرسال تعليق